• HABARI MPYA

  Jumatatu, Juni 25, 2012

  HII NDIYO FIRST ELEVEN YA ROBO FAINALI EURO 2012


  Cristiano Ronaldo - Portugal
  RONALDO
  NUSU Fainali zimejulikana baada ya mechi za Robo Fainali na kuna wachezaji ambao walionyesha viwango baab kubwa, kiasi cha kuzibeba timu zao katika hatua hiyo.

  Langoni, Gianluigi Buffon aliokoa penalti ya Ashley Cole katika mikwaju mitano mitano usiku wa jana.

  Katika beki, Glen Johnson alifanya vema katika mechi na Azzurri, wakati Pepe alisimama imara kwenye safu ya ulinzi ya Ureno, na hakuwaruhusu Czech kupiga mashuti ya kulenga lango. Mats Hummels alikuwa kizingiti katika ushindi wa Ujerumani wa 4-2 dhidi ya Ugiriki, wakati Jordi Alba alifanya vitu adimu katika kuzuia na kushambulia wakati Hispania ikiifunika Ufaransa.
  Xabi Alonso alicheza mechi yake ya 100 huku akichangia kwa kiasi kikubwa La Roja kutinga Nusu Fainali. Andrea Pirlo amedhihirisha kuwa 'mapigo ya moyo' wa Italia kwa mara nyingine, akiumiliki vema mchezo dhidi ya England, kisha akafunga mkwaju wake wa penalti. Mtu mwingine aliyecheza soka baab kubwa kwa Ujerumani ni Sami Khedira, ambaye aling'ara dhidi ya Ugiriki.
  Marco Reus na Miroslav Klose nao walikuwa hatari, wote walifunga mabao mazuri katika ushindi wa Ujerumani. Miwsho, Cristiano Ronaldo alikuwa shujaa wa Ureno kwa mara nyingine, akiipeleka timu yake Nusu Fainali kwa mabao ya kichwa. BIN ZUBEIRY kwa msaada wa Goal.com inakupa sasa wachezaji 11 wa kuunda kikosi bora cha Robo Fainali za Euro 2012.

  BUFFON
   ITALIA

  JOHNSONPEPEHUMMELSJORDI ALBA
  ENGLAND
  URENOUJERUMANIHISPANIA

  XABI ALONSOPIRLOKHEDIRA
   
  HISPANIA ITALIAUJERUMANI

  REUSKLOSERONALDO
   
  UJERUMANI
  UJERUMANIURENO
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HII NDIYO FIRST ELEVEN YA ROBO FAINALI EURO 2012 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top