• HABARI MPYA

    Monday, June 25, 2012

    BEKI LIVERPOOL AFARIKI DUNIA KWA SARATANI


    BEKI wa Real Betis, Miki Roque amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 23 baada ya kusumbuliwa na maradhi ya saratani.
    Roque, ambaye aliibuliwa katika programu ya vijana ya Liverpool kabla ya kurejea nyumbani kwao kujiunga na Betis, alifanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye fupanyonga yake mwaka jana.
    Miki Roque spent four years at Liverpool
    Miki Roque enzi zake  Liverpool
     
    Taarifa ya tovuto ya Betis imesema jana: 'Mchezaji wa The Real Betis Miquel Roque Farrero, Miki Roque, amefariki leo katika hospitali ya Instituto Dexeus, Barcelona akiwa ana umri wa miaka 23.
    'Miki Roque amekuwa akisumbuliwa na saratani tangu Machi 2011, Real Betis inawasilisha salamu za rambirambi kwa familia ya Roque.'
    Devastated: Miki Roque wept as he announced his retiredment from football
    Miki Roque akimwaga machozi wakati akitangaza kustaafu kwa sababu ya saratani

    Roque alikaa miaka minne Liverpool kati ya mwaka 2005 na 2009 na aliisaidia klabu hiyo kutwaa Kombe la FA la Vijana mwaka 2006. 
    Aliingia akitokea benchi kwenye kikosi cha kwanza katika mechi dhidi ya Galatasaray katika Ligi ya Mabingwa Ulaya Desemba mwaka 2006.
    Akiwa Anfield, Roque alipelekwa kwa mkopo Oldham na klabu za Hispania,  Xerez na Cartagena kabla ya kuhamia moja kwa moja Betis mwaka 2009, akiichezea mechi ya kwanza klabu hiyo ya Hispania Oktoba 2010.
    Taarifa ya A Liverpool imesema: 'Liverpool FC leo imepokea habari za kusikitisha kwamba mchezaji wake wa zamani Miki Roque amepolteza maisha yake kwa ugonjwa wa saratani akiwa ana umri wa miaka 23.
    'Kila mmoja katika Liverpool angependa kuwapa pole familia ya Miki katika kipindi hiki cha majonzi.'

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BEKI LIVERPOOL AFARIKI DUNIA KWA SARATANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top