• HABARI MPYA

  Jumapili, Juni 24, 2012

  KIGGI MAKASSY AANZA KUIPIGIA MABAO SIMBA


  Kiggi Makasy- nyota wa mchezo
  Simba v Express leo
  Na Princess Asia
  KIUNGO mpya wa Simba SC, Kiggi Makassy leo ameifungia bao lake kwanza klabu hiyo, tangu ajiunge nayo mwezi huu kutoka kwa mahasimu, Yanga. Kiggi, aliifungia Simba bao lililoelekea kuwa la ushindi dakika ya 20 katika mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Uganda, Express ‘Tai Mwekundu’ kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
  Hata hivyo, bao hilo la Kiggi lilidumu kwa dakika 20 tu, kwani dakika ya 40, Joseph Kaira aliwasawazishia Tai Wekundu na hadi kipyenga cha mwisho, timu hizo zilitoka 1-1.
  Jana mabingwa hao wa Ligi Kuu waliiichapa Toto African ya Mwanza mabao 2-0 katika mechi kali ya kirafiki iliyofanyika Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
  Wakati huo huo: Kocha Mkuu wa Simba, Mserbia Milovan Cirkovic anatarajiwa kutua saa 8:45 usiku kutoka nyumbani kwao, Serbia alikokuwa kwa mapumziko. Milo atatua na na dege la shirika la ndege la Uturuki.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIGGI MAKASSY AANZA KUIPIGIA MABAO SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top