• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 27, 2012

  MASOMBO LINO AWAPAGAWISHA SIMBA TCC


  Masombo Lino kulia, baada ya kumpokonya mpira Kiggi kama alimuazima, akitaka kugeuka kusukuma mashambulizi, Uwanja wa TCC jana. Jamaa ni mzuri kwa kweli na Simba watamsahau Yondan.

  Na Prince Akbar
  BEKI wa Simba SC, Masombo Lino Masombo Lino kutoka Daring Club Motema Pembe kutoka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), jana alikuwa kivutio kikubwa katika mazoezi ya klabu hiyo, Uwanja wa TCC, Chang’ombe, Dar es Salaam.
  Katika mazoezi yaliyoongozwa na Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mserbia Milovan Cirkovick, Masombo alionyesha ni mzuri kwenye kuzuia na kusaidia mashambulizi pia.
  Mashabiki wa Simba walikuwa wenye furaha kubwa TCC jana kutokana na mavituuz yaliyokuwa yakifanywa na wachezaji wao wengine wapya pia.
  Mazoezi ya Simba yanaendelea leo kwenye Uwanja huo, kujiandaa na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, michuano iliyopangwa kuanza Julai 14 hadi 29, mwakani.
  Beki hilo la kati ambalo lilipiga soka ya uhakika mwaka jana wakati Simba ilipokutana na DC Motema Pembe katika mechi ya mchujo kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika lilitua jana Dar es Salaam na leo imeelezwa limesaini mkataba. 
  Simba, mabingwa wa Ligi Kuu ya Bara, wamemsajili beki huyo kuziba pengo la beki wao hodari, Kelvin Patrick Yondan ambaye amehamia kwa wapinzani, Yanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MASOMBO LINO AWAPAGAWISHA SIMBA TCC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top