![]() |
| Uwanja wa Old Trafford unaotarajiwa kuipa tuzo Man United FC |
KLABU ya Manchester United imeingizwa
kwenye kinyang’amyiro cha tuzo nne kutokana na kuboresha, bidhaa na maendeleo
kwa ujumla na kupanua soko lake.
Tuzo tatu za awali ni Tuzo za Biashara
ya Uwanja, ambazo zitafanyika mjini Turin, Italia, Mei 15. Tuzo hizo
zilianzishwa mwaka 2010, zinahusu mafanikio, ukarabati na fikra safi
zinazoendana na dunia ya viwanja, utawala na uboreshaji wa maeneo ya michezo.
Manchester United imeingizwa
kuwania tuzo ya Mradi Bora wa Mwaka kwa kuendeleza eneo la jukwaa la vyumba la West
Stand.
Ubora wa mradi huo kwamba ni wa kisasa
mno na umefanywa kuwa na vifaa ambavyo vinawawezesha mashabiki kujisikia raha
wawapo eneo hilo na kuanzisha pia jukwaa lingine la maraha kwa ajili ya ‘watu
wazito’ lenye mazingira ya kuvutia ile mbaya.
Klabu hiyo pia imetajwa katika
kuwania tuzo ya Ubora wa uhakika, ambayo inahusu mafanikio kwa ujumla, mafanikio
ya uongozi katika matukio mbalimbali.
Manchester United inatumai
kukomba tuzo zote hizo tatu na kuwa klabu ya kwanza Uingereza, Uwanja wake kumiliki heshima zote
kubwa hizo tatu.
Gwiji wa Manchester United, Gary
Neville, ambaye hivi karibuni alipewa heshima ya Balozi wa Mazingira wa klabu,
alisema: “Ni babu kubwa kuona Manchester United imepata heshima hii katika
utawala wa mazingira. Nafahamu klabu ina jukumu kubwa la kuboresha zaidi mambo,”alisema.



.png)
0 comments:
Post a Comment