• HABARI MPYA

  Saturday, December 08, 2018

  MWADUI FC YAITANDIKA ALLIANCE YA MWANZA 4-0 NA NDANDA FC YALAZIMISHWA SARE 0-0 NA TANZANIA PRISONS NANGWANDA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Mwadui FC imeutumia vyema Uwanja wa nyumbani, Mwadui Complex wilayani Kishapu mkoani Shinyanga baada ta kuichapa mabao 4-0 Alliance FC ya Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo.
  Ushindi huo umetokana na mabao ya Ottu Samuel Joseph mawili dakika za 33 na 85 na ean Marie Girukwishaka dakika ya 40 na  Ibrahim Irakoze dakika ya 62.
  Mwadui FC inafikisha pointi 17 baada ya ushindi huo katika mechi yake ya 16 ya msimu na kujiinua kwa nafasi tatu hadi ya 12 kwenye Ligi Kuu ya timu 20, wakati Alliance FC inabaki nafasi ya 17 kwa pointi zake 13 za mechi 16.

  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Ndanda FC imelazimishwa sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons ya Mbeya Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
  Ndanda inafikisha pointi 15 kwa sare hiyo baada ya kucheza mechi 16, ikiendelea kushika nafasi ya 16, wakati Tanzania Prisons inafikisha pointi 11 baada ya kucheza mechi 16 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya 18 ikiihamishia mkiani Biashara United ya Mara yenye pointi 10 za mechi 14. 
  African Lyon inashika nafasi ya 19 sasa kwa pointi zake 11 baada ya kucheza mechi 15, ikiwa inazidiwa tu wastani wa mabao na Ndanda FC.
  Ligi Kuu itaendelea kesho kwa michezo miwili, Yanga SC wakiikaribisha Biashara United Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam na Coastal Union wakiwa wenyeji wa Mbeya City Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga kuanzia Saa 10:00 jioni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWADUI FC YAITANDIKA ALLIANCE YA MWANZA 4-0 NA NDANDA FC YALAZIMISHWA SARE 0-0 NA TANZANIA PRISONS NANGWANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top