• HABARI MPYA

  Friday, February 05, 2016

  TFF YAWAWEKA MTEG0 BOMU 'WAUZA NA WANUNUA MECHI LIGI KUU...MAREFA 'WAKUDA' NAO KUKIONA

  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeweka mtego maalum kuwanasa watu wanaojihusisha na upangaji wa matokeo katika michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kuanzia wachezaji, marefa na wasimamizi.
  Mtego huo unahusu pia mashindano mengine yote nchini, ikiwemo Daraja la Kwanza (FDL), Daraja la Pili (SDL) na Kombe la Shirikisho, maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
  Rais wa TFF, Jama Malinzi ambayo imeonya juu ya upangaji matokeo nchini

  Taarifa ya TFF kwa BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE leo imesema kwamba shirikisho hilo limejipanga vizuri kusimamia kwa umakini mashindano yake yote yanayoendelea nchini.
  Na taarifa hiyo imesema kwamba yeyote atakayebainika kujihusisha na mchezo huo wa upangaji matokeo atachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
  "Katika michezo yote inayoendelea TFF ina maofisa wake wanaofuatilia kwa ukaribu michezo hiyo, hivyo endapo kiongozi, mchezaji, msimamizi au mwamuzi atabainika kujihusisha na upangaji wa matokeo hatua kali zitachukuliwa,"imesema taarifa ya TFF na kuongeza.
  "TFF inawaomba viongozi, wachezaji, wasimamizi wa michezo na waamuzi kutojihusisha na mchezo huo wa upangaji wa matokeo kwani kufanya hivyo ni kukiuka katiba, sheria na kanuni zinaongoza mpira wa miguu nchini,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YAWAWEKA MTEG0 BOMU 'WAUZA NA WANUNUA MECHI LIGI KUU...MAREFA 'WAKUDA' NAO KUKIONA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top