• HABARI MPYA

  Wednesday, December 01, 2021

  SIMBA SC YAICHAPA GEITA GOLD 2-1 DAR


  MABINGWA watetezi, Simba SC wameendeleza furaha kwa mashabiki wao baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na viungo, Mmalawi Peter Banda dakika ya tisa na mzawa, Muzamil Yassin dakika ya 57, wakati la Geita Gold limefungwa na kiungo pia, Juma Mahadhi dakila ya 66.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 17, ingawa inabaki na nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na watani wa jadi, Yanga SC baada ya timu zote kucheza mechi saba kuelekea mechi baina yao Desemba 11 hapo hapo Mkapa.
  Geita Gold yenyewe baada ya kichapo cha leo inabaki na pointi zake tano za mechi saba pia katika nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16, ikiizidi pointi tatu tu Mtibwa Sugar inayoshika mkia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAICHAPA GEITA GOLD 2-1 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top