• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 27, 2019

  WACHEZAJI 40 WAITWA KIKOSI CHA AWALI CHA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya wanawake, Twiga Stars Bakari Nyundo Shime ametaja kikosi cha wachezaji 40 watakaoingia kambini kujiandaa na mashindano mbalimbali.
  Kikosi hicho kitakachoingia kambini rasmi Agosti 30 hadi Septemba 21mwaka huu kinaundwa na Najat Abas (JKT), Tausi Abdallah (Mlandizi), Zubeda Mgunda (Simba), Stumai Abdallah (JKT) na Wema Richard (Mlandizi).
  Wengine ni Enekia Kasonga (Alliance), Vailet Thadeo (Simba), Fatuma Issa (Evergreen), Vailet Singano (Simba), Happy Hezron (JKT), Janeth Christopher (Mlandizi), Eva Wailes (Ruvuma) na Amina Ally (Simba).
  Wamo pia Diana Lucas (Ruvuma), Asha Hamza (Kigoma), Pheromena Daniel (Mlandizi), Opa Clement (Simba), Herieth Shija (Mash Academy), Donisia Minja (JKT), Joyce Fredy (Tanzanite) na Janeth Shija (Simba).
  Wengine ni Masha Omari (Panama), Ester Mabanza (Alliance), Anastazia Nyandago (Panama), Rahabu Joshua (Alliance), Dotto Tossy (Simba), Neema Charles (Panama), Lucia Mrema (Panama) na Wande Mahona (Tabora).
  Wamo pia Fumukazi Ally (JKT), Emeliana Mdimu (Makongo Sec), Protasia Mbunda (Ruvuma), Irene Kisisa (Kigoma), Shamimu Ally (Ruvuma), Joyce Meshack (Makongo Sec), Thadea Hamdani (Yanga), Rukia Hussein (Tanzanite), Aisha Masaka (Alliance), Agnes Palangyo (Tanzanite) na Angel Joseph (Arusha).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WACHEZAJI 40 WAITWA KIKOSI CHA AWALI CHA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top