• HABARI MPYA

    Friday, August 30, 2019

    KABWILI NA ALLY NG’ANZI WAITWA KIKOSI CHA BARA CHINI YA MIAKA 20 KUCHEZA CECAFA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Zuberi Katwila ameita wachezaji 35 katika kikosi cha awali kujiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA U20) itakayofanyika Septemba mwaka huu nchini Uganda. 
    Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kutaja kikosi hicho leo mjini Dar es Salaam, Katwila ambaye pia ni Kocha Mkuu wa klabu ya Mtibwa Sugar alisema kwamba kikosi hicho kitaingia kambini Jumatatu.
    Aliwataja wachezaji wanaounda kikosi hicho ni makipa; Ramadhani Kabwili wa Yanga SC, Ally Salim wa Simba SC na Abdul Suleiman aliyepandishwa kutoka kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys.



    Kipa wa Yanga SC, Ramadhani Kabwili ameitwa kikosi cha U20 kwa ajili ya michuano ya CECAFA 

    Mabeki ni; Nickson Kibabage (Difaa Hassan El-Jadidi, Morocco), Oscar Maasai (Azam FC), Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Dickson Job (Mtibwa Sugar), Gustapha Simon (Yanga SC), Onesmo Mgaya (Mtibwa Sugar), James Kahimba (Coastal Union), Ally Msengi (KMC) na Kelvin Kijiri (KMC).
    Viungo ni Ally Ng’anzi (Madson, Marekani), Kelvin Nashon (JKT), Lenny Kissu (Biashara United), Yahya Mbegu (Simba SC), Frank Kahole (Mtibwa Sugar), Andrew Simchiba (Coastal Union), Kibwana Shomari (Mtibwa Sugar), Tariq Seif (Biashara United), Zanda Said (Azam FC), Tepso Evance (Azam FC) na Herbert Lukindo (Mbao FC).
    Washambuliaji ni Mohammed Abdallah (Mtibwa Sugar), Razack Ramadhani (Mtibwa Sugar), Wilbore Maseke (Azam FC), Gadafi Said (Azam FC), Novatus Dissmas (Biashara United), Abubakar Juma (Mtibwa Sugar), Israel Mwenda (Alliance FC), Samuel Jackson (Azam FC), Omar Banda (Azam FC), Kassim Shaaban (Sahare FC), Agiri Ngoda (Azam FC) na Kelvin John (U17).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KABWILI NA ALLY NG’ANZI WAITWA KIKOSI CHA BARA CHINI YA MIAKA 20 KUCHEZA CECAFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top