• HABARI MPYA

  Jumapili, Agosti 18, 2019

  YANGA SC YAAMSHA MATUMAINI, YAWAPIGA AFC LEOPARDS 1-0 MECHI YA KIRAFIKI ARUSHA

  Na Mwandishi Wetu, ARUSHA
  YANGA SC imeamsha kidogo matumaini ya mashabiki wake baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya AFC Leopards ya Kenya katika mchezo wa kirafiki jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
  Ushindi wa leo umetokana na bao la Nahodha, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Papy Kabamba Tshishimbi aliyefunga kwa kichwa dakika ya 83 akimalizia kona ya kiungo mwenzake, Mnyarwanda Patrick ‘Papy’ Sibomana kutoka kulia. 
  Na hiyo ilifuatia Yanga kutawala vizuri mchezo na kupeleka mashambulizi mengi langoni mwa Leopards, lakini tu wakakosa mipango au bahati ya kutumbukiza mpira nyavuni.
  Leopards, zamani ikijulikana kama Abaluhya ilimaliza pungufu baada ya mchezo wake, Vincent Oburu kutolewa kutolewa kwa kadi nyekundu dakia ya 90 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kutokana na kumchezea rafu Tshishimbi. 
  Kadi ya kwanza ya njano alionyeshwa mapema kipindi cha kwanza baada ya kumchezea rafu beki wa kulia wa Yanga, Paul Godfey ‘Boxer’.
  Huu unakuwa mchezo wa sita Yanga wanashinda msimu huu, baada ya awali baada ya awali kushinda 4-1 dhidi ya Mlandege visiwani Zanzibar, 2-0 dhidi ya Friends Rangers, 7-0 dhidi ya ATN, 2-0 dhidi ya Moro Kids na 1-0 dhidi ya Mawenzi Market zote mjini Morogoro n azote zikiwa za kirafiki pia.
  Mechi nyingine, walifungwa 2-0 na Polisi 2-0 mjini Moshi na kutoa sare za 1-1 dhidi ya Malindi SC ya Zanzibar na Kariobangi Sharks ya Kenya zote za kirafiki na 1-1 pia dhidi ya Township Rollers ya Botswana Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Baada ya mchezo wa leo, Yanga itasafiri usiku wa kuamkia kesho kwenda Gaborone nchini Botswana kupitia Johannesburg nchini Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa marudiano na wenyeji, Township Rollers wakihitaji ushindi wa ugenini ili kusonga mbele.
  Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Metacha Mnata, Paul Godfrey ‘Boxer’, Ally Mtoni ‘Sonso’, Lamine Moro, Kelvin Yondan, Papy Tshishimbi, Mapinduzi Balama, Mohamed Issa ‘Banka’, Sadney Urikhob/Mrisho Ngassa dk72, Juma Balinya/David Molinga ‘Falcao’ dk73 na Patrick Sibomana/Issa Bigirimana dk87.
  AFC Leopards; Benjamin Ochan, Dennis Sikhayi, Isaac Kipyegon, Christopher Orochum, Soter Kayumba, Eugene Mukangula/Vincent Mabamahoro dk75, Jaffar Owiti/Boniphace Mukhekhe dk72, Tresor Ndikumana, Ismaila Diara/Hansel Ocheng dk80, Whyvonne Isuza na Vincent Oburu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YAAMSHA MATUMAINI, YAWAPIGA AFC LEOPARDS 1-0 MECHI YA KIRAFIKI ARUSHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top