• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 20, 2019

  AZAM FC DHIDI YA FASIL KENEMA KIINGILIO NI KUANZIA SH 3,000 MZUNGUKO HADI 10,000 VIP

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Azam FC imetaja viingilio vya mchezo wake wa marudiano Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Fasil Kenema ya Ethiopia Jumamosi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
  Azam FC inayofundishwa na kocha Mrundi, Ettienne Ndayiragijje inahitaji ushindi wa kuanzia 2-0 ili kusonga mbele baada ya kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza nchini Ethiopia.
  Na kuelekea mchezo wa marudiano Jumamosi, leo klabu imetajaa viingilio huku kiingilio cha chini kabisa ni Sh. 3,000 kwa jukwaa la mzunguko.

  Mshambuliaji tegemeo wa Azam FC, Shaaban Iddi Chilunda mazoezini leo kuelekea mechi na Fasil Kenema

  Viingilio vingine vya mchezo huo ni Sh. 10,000 kwa VIP A na VIP B na Sh. 5,000 kwa VIP C, wakati tiketi zitaanza kuuzwa Alhamisi.
  Tiketi hizo zitauzwa katika vituo vya Magomeni Azam Ice Cream Center, Azam Shop Kariakoo, Mbagala Rangi Tatu na uwanjani siku ya mechi, ambayo mlangoni kila mtu atapatiwa Azam Ukwaju Ice Cream bure.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC DHIDI YA FASIL KENEMA KIINGILIO NI KUANZIA SH 3,000 MZUNGUKO HADI 10,000 VIP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top