• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 29, 2019

  SIMBA SC YAANZA VYEMA LIGI KUU, YAWACHAPA JKT TANZANIA 3-0 KAGERE AANZA NA MBILI

  Na Saada Salim, DAR ES SALAAM
  MABINGWA watetezi, Simba SC wameanza vyema msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Tanzania jioni ya leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  Mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda, Meddi Kagere alikaribia kufunga hat trick katika mechi ya kwanza baada ya kufunga mabao mawili, huku lingine likifungwa na Miraj Athumani ‘Madenge’ aliyerejeshwa kikosini msimu huu.
  Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems leo aliwaanzisha wachezaji wapta, Wabrazil Tairone Santos na Gerson Fraga kucheza pamoja safu ya ulinzi kwa mara ya kwanza tangu wasajiliwe Julai na wakafanya vizuri.


  Kagere aliye katika msimu wake wa pili Msimbazi tangu asajiliwe kutoka Gor Mahia ya Kenya, alifunga bao la kwanza sekunde ya 20 ya dakika ya kwanza akimalizia pasi ya kiungo Hassan Dilunga kabla ya kufunga la pili dakika ya 59 akimalizia pasi ya kiungo mwingine mzawa, Muzamil Yassin.
  Kagere alikaribia kukamilisha hat trick dakika ya 65 kama si shuti lake kugonga mwamba – lakini dakika 73 akamtilia krosi nzuri mtokea benchi Madenge aliyefunga kwa kichwa kuipatia Simba SC bao la tatu.
  Edward Songo aliyetokea benchi pia akaifungia bao la kufutia machozi JKT Tanzania dakika ya 87 kwa shuti la umbali wa mita 25 lililompota kipa namba wa Simba na timu ya taifa ya Tanzania, Aishi Salum Manula.
  Kikosi cha JKT Tanzania kilikuwa; Abdulrahman Mohammed, Madenge Ramadhani/Michael Aidan dk64, Edward Charles, Mohammed Fakh, Rahim Juma, Jabir Aziz, Mwinyi Kazimoto, Hafidh Mussa, Hassan Matalema/Said Luyaya dk79, Danny Lyanga na Ally Bilal/EdwardSongo dk62.
  Simba SC: Aishi Manula, Haruna Shamte, Mohammed Hussein, Erasto Nyoni,  Tairone Santos, Gerson Fraga, Deogratius Kanda/Miraj Athumani dk60, Muzamil Yassin, Meddie Kagere, Hassan Dilunga/Sharaf Shiboub dk71 na Clatous Chama/Ibrahim Ajibu dk78.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAANZA VYEMA LIGI KUU, YAWACHAPA JKT TANZANIA 3-0 KAGERE AANZA NA MBILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top