• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 24, 2019

  MALINDI SC KUMENYANA NA AL MASRY BAADA YA KUWAOTA MOGADISHU CITY LEO AMAAN

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  TIMU ya Malindi SC ya Zanzibar imefanikiwa kwenda Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Mogadishu City ya Somalia jioni ya leo Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar.
  Matokeo yanamaanisha Malindi SC inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 1-0 kufuatia wiki mbili zilizopita kulazimishwa sare ya 0-0 na Wasomali hao hapo hapo Uwanja wa Amaan.
  Shujaa wa Malindi SC leo alikuwa ni mshambuliaji wake tegemeo, Mohammed Mossi aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 67 na sasa wawakilishi hao wa Zanzibar watamenyana na Al-Masry ya Misri katika hatua inayofuata.
  Mechi zote za Raundi ya kwanza baina ya timu hizo zilicheza Zanzibar kutokana na ombi la Mogadishu City wenyewe.
  Kwenye Raundi ya pili, Malindi SC wataanzia nyumbani tena kati ya Septemba 13 na 15, kabla ya kusafiri kwenda Misri kwa mchezo wa marudiano kati ya Septemba 27 na 29.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MALINDI SC KUMENYANA NA AL MASRY BAADA YA KUWAOTA MOGADISHU CITY LEO AMAAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top