• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 23, 2019

  TIMU YA VIJANA YA TANZANIA YACHAPWA 2-1 NA RWANDA MICHUANO YA CECAFA U15

  Na Mwandishi Wetu, ASMARA
  TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania leo imejiweka kwenye nafasi ngumu ya kwenda Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya umri wa miaka 15 (CECAFA U15) baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Rwanda mjini Asmara, Eritrea  
  Katika mchezo wa leo, mabao ya Rwanda yamefungwa na Hoziraya Kenedy dakika ya tano na Irahamye Eric dakika ya 33, wakati la Tanzania limefungwa na Rabin Sanga kwa penalti dakika ya nane.
  Baada ya kucheza mechi tatu, ikifungwa mbili, nyingine ilipigwa 2-0 na Uganda na kushinda moja 6-0 dhidi ya Sudan Kusini nafasi ya Tanzania kwenda Nusu Fainali ni kama haipo kutokana na mwenendo mzuri wa Uganda na Rwanda.
  Na baada ya mchezo wa leo, Tanzania inayofundishwa na mchezaji wa zamani wa Yanga, Maalim Saleh ‘Romario’ itarudi uwanjani kwa ajili ya mechi yake ya mwisho ya Kundi B kwa kumenyana na Ethiopia Jumapili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TIMU YA VIJANA YA TANZANIA YACHAPWA 2-1 NA RWANDA MICHUANO YA CECAFA U15 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top