• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 15, 2019

  MWAKA 2003 ULIVYOMUIBUA MCHEZAJI ATHUMANI IDD 'CHUJI'


  Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM
  WANASEMA ya kale dhahabu ni msemo wenye maana sana japo wengi tunashindwa kuuelewa lakini pia huwezi kufanikiwa zaidi bila kuangalia walio kutangulia. Katika soka letu leo nimeamua kumzungumzia mmoja kati ya viungo bora kabisa ambao niliwahi kuwashuhudia naweza kusema ni vipaji adimu sana bila kujali kama alifanikiwa kwa upande mwingine wa maisha ya kawaida au laah mimi nimetamani kuuzungumzia ujuzi wake uwanjani na akili kubwa ambayo Mungu alimjalia akiwa katika dimba la chini kiungo mkabaji,mwenye umiliki maridadi wa mpira huku akipiga pasi hapa nilipo na Kariakoo na ikafika kwa mlengwa kuna wakati unaweza tamani hata kurudisha zama ili vijana wa leo waone ila wanasemaga wakati ukuta. Ni Athumani Idd wengi hupenda kumuita Chuji.
  Kiungo huyu aliyeanza soka lake kunako klabu ya Polisi Dodoma,Chuji alitokea kuwa mlinzi bora wa kati Tanzania,alikuwa akipata nafasi ya kucheza timu ya Taifa ya vijana "Serengeti Boys" ,Mwaka 2005 akitokea timu za nje ya Dar- es- salaam na kupata nafasi moja kwa moja kunako timu ya Taifa ya vijana.
  Namba tano mwenye sifa zote akiwa uwanjani, mwenye utulivu wa hali ya juu,mpangaji mzuri wa ngome yake,kiongozi ,akiwa katika nafasi ya ulinzi wa kati ambayo alikuwa akicheza katika timu yake ya Polisi Dodoma,mara baada ya kuja Simba alikuta nafasi hiyo inawatu zaidi ya yeye,kama vile wakina Victor Costa,na beki mrundi Said Koko'o hivyo kwake ilikuwa ngumu sana kupata namba chini ya hao watu.

  ALITUMIA NAFASI NA KUONYESHA UWEZO WAKE 
  Utovu wa nidhamu wa baadhi ya wachezaji wa Simba kama Victor Costa ,Chuji alitumia nafasi hiyo alipopewa nafasi ya kucheza na kuonesha uwezo wake wa hali ya juu hadi kupelekea kumshawishi aliyekuwa kocha mkuu wa Simba mwaka huo "Neidor Dos Santos" na ndiyo hapo hapo Chuji alipomwaminisha kocha Huyo kuwa yeye anaweza, Santos alipendezwa sana na viwango walivyoonesha vijana waliopewa nafasi katika mechi hiyo kama vile Henry Joseph, Kelvin Yondani,na Chuji mwenyewe,mara baada ya wachezaji wake wakina Victor kumuonyesha utovu wa nidhamu.

  YANGA WAKAMUONA
  Soka la uhakika akicheza katika idara ya kiungo kwa dakika 120 lilimtambulisha kiungo huyo na kupewa Jina " mapafu ya mbwa"Japo alikosa penati mchezo huo wa nusu fainali mara baada ya mchezo huo kuisha kwa sare ya bao 1-1 uliowakutanisha Simba Na Yanga.
  AKASAJILIWA YANGA NA KUWABEZA SIMBA ILIYOMTAMBULISHA KATIKA RAMANI YA SOKA TANZANIA:
  Kauli kali aliyoitoa aliposajiliwa kwenda Yanga " kurudi Simba bora akauze ndimu "
  NINI KILIENDELEA NA BAADAE ALIRUDI KWA WEKUNDU WA MSIMBAZI SIMBA NA WALIMPOKEA LICHA YA KAULI YAKE HIYO.
  (Dominick Salamba ni mchambuzi wa soka anapatikana pia kupitia katika Akaunti yake ya Instagram kama @dominicksalamba au namba +255713942770)
  Itaendela•••
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MWAKA 2003 ULIVYOMUIBUA MCHEZAJI ATHUMANI IDD 'CHUJI' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top