• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 28, 2019

  JACKPOT KUBWA YA KIHISTORIA YA TANZANIA, SH MILIONI 825 ZAKABIDHIWA KWA WASHINDI WAWILI KUTOKA SPORTPESA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BAADA ya Jackpot ya SportPesa kuvunjwa kwa mara ya kwanza ikiwa imefikia jumla ya milioni 825,913,640/= na washindi wawili kupatikana,leo hii wamekabidhiwa rasmi mkwanja wao kila mmoja akichomoka na kitita cha milioni 412,956,820/= baada ya kubashiri kwa usahihi mechi kumi na tatu za Jackpot wiki iliyopita.
  Kingsley Simon Pascal mwenye umri wa miaka 26 akitokea Biharamlo ndiye mshindi  wa kwanza wa Jackpot na mshindi mwingine ni Magabe Matiko Marwa mwenye miaka 31 akitokea wilaya ya Serengeti wote wakigawana kwa usawa kitita hicho cha Jackpot.
  Mkurugenzi wa utawala na udhibiti wa SportPesa ndugu Tarimba Abbas akizungumza wakati wa kuwakabidhi hundi kwa washindi hao wa kihistoria alisema,” Nafurahia kuwakabidhi  washindi wetu wa shilingi milioni 825,913640/= za Jackpot yetu ambayo ndiyo kubwa zaidi nchini,ni hii ikiwa ni mara ya kwanza kwenye historia ya betting Tanzania kwa kiasi kama hichi kutolewa kwa washinidi wa michezo ya kubahatisha aliendelea kwa kusema “‘’Naomba mtambua kila wiki watu wanacheza michezo mbali mbali na Sportpesa ila kwenye hii segment ya Jackpot tangu tumeanza tumetoa zaidi ya bilioni 4.4 kwa washindi na kati pesa hizi kodi ni million 864 na hutujawahi kupata malalamiko kutoka kwa washindi wetu na wamekuwa wakituamini na kuwa na uhakika wa kushinda.’’
  Kwa upande wa washindi kila mmoja akionyesha furaha ya kipekee wakifurahia ushindi wao, na wote wakikiri kuwa iliwachukua muda kuamini kama kweli pesa zote hizo ni za kwao, Magabe Matiko Marwa ambaye pia ni mshindi wa Bonus za Jackpot wiki iliyopita akiwa na mke wake Bi Elizabeth Wambura alionekana kuwa na furaha isiyo ya kawaida kabisa.

  “Leo ndio nimeamini rasmi mara baada ya kukabidhiwa fedha hizi na kuamini kwa macho yangu kama nimeshinda, naomba watanzania waamini kuwa mimi nimeshinda kweli na si vinginevyo.”
  “Watanzania waamini mimi sifahamiani na mtu yoyote SportPesa na kuibuka mshindi niliweka mkeka mmoja wa shilingi 2000/= tu”
  Kingsley alipoulizwa kuhusu watu wasioamini kama wanaweza kushinda alisema,’’ huwezi kupata kitu usipojaribu na mimi ni mtu wa kujaribu vitu vingi na sasa ni mshindi wa Jackpot nachoweza kusema kila mtu anaweza kushinda akijiamini na kuweka nia bila kukata tamaa”
  “Tangu nianze kubet Jackpot mwezi wa tatu mwaka huu hii ni mara ya 17 kama si 16 na nimebahatika kuibuka mshindi wa mil 412,956,820/=”
  Changamkia fursa kwa kucheza Jackpot mpya ya SportPesa dau likiwa milioni 200 kwa kupiga *150*87# au temebelea www.sportpesa.co.tz.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: JACKPOT KUBWA YA KIHISTORIA YA TANZANIA, SH MILIONI 825 ZAKABIDHIWA KWA WASHINDI WAWILI KUTOKA SPORTPESA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top