• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 16, 2019

  HERI SASII, KOMBA, MKONO NA JEONESIYA RUKYAA KUCHEZESHA MECHI YA NGAO KESHO

  Na Asha Said, DAR ES SALAAM              
  REFA Heri Sasii ndiye atakayechezesha mechi ya Ngao ya Jamii baina ya Simba SC na Azam FC kesho kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo amesema kwamba Sasii atasaidiwa na Frank Komba, wote wa Dar es Salaam na Mohammed Mkono kutoka Tanga ambao wote watakuwa wakishika vibendera.
  Ndimbo amesema kwamba wengine watakuwa ni refa wa akiba, Ferdinand Chacha wa Mwanza atayekuwa mezani na Jeonisiya Rukyaa pamoja na Martin Saanya watakaokuwa waamuzi wasaidizi pande zote za milango. Amesema maandalizi yamekamilika na ulinzi utakuwa wa kutosha.
  Makocha wote, Mbelgiji Patrick Aussems wa Simba SC na Mrundi, Etienne Ndayiragijje wa Azam FC waliwakilishwa na wasaidizi wao.  
  Kocha wa makipa wa Simba, Muharami Muhammed ‘Shilton’ alisema kikosi chao kipo vizuri na wanataraji kuendeleza ubabe kesho, wakati kocha Msaidizi wa Azam FC, Iddi Nassor Cheche naye alisema kikosi chao kipo vizuri na ushindi lazima kesho.
  Lakini Muharami aliwataja wachezaji wawili ambao wataukosa mchezo huo ni kipa Aishi Manula na kiingo Ibrahim Ajibu sawa na Azam FC ambao Cheche alisema wana majeruhi wawili pia ni beki Aggrey Morris na kiungo Mudathir Yahya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HERI SASII, KOMBA, MKONO NA JEONESIYA RUKYAA KUCHEZESHA MECHI YA NGAO KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top