• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 21, 2019

  TANZANIA YAPATA USHINDI WA KWANZA MICHUANO YA CECAFA U15, YAIPIGA SUDAN KUSINI 6-0

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania leo imepata ushindi wa kwanza kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya umri wa miaka 15 (CECAFA U15) baada ya kuichapa Sudan Kusini mabao 6-0 mjini Asmara, Eritrea  
  Katika mchezo huo wa Kundi B, mabao ya Tanzania inayofundishwa na kocha Maalim Saleh ‘Romario’ yamefungwa na Hashim Kiambe 26, Rabin Sanga mawili, moja kwa penalti dakika ya 36 na lingine dakika ya 70, Fundumo Joseph mawili dakika za dakika ya 40 na 55 Fundumo Joseph na Ladaki Juma dakika ya 80.
  Na hiyo inafuatia timu hiyo kuanza vibaya michuano hiyo baada ya kufungwa 2-0 na Uganda, mabao ya Travis Mutyaba dakika ya 27 na 80 mjini Asmara, Eritrea  
  Baada ya mchezo wa leo, Tanzania itarudi uwanjani kwa mechi zake mbili za mwisho za Kundi B, dhidi ya Rwanda na Ethiopia kuangalia iwezekano wa kusonga mbele.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TANZANIA YAPATA USHINDI WA KWANZA MICHUANO YA CECAFA U15, YAIPIGA SUDAN KUSINI 6-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top