• HABARI MPYA

  Jumapili, Agosti 11, 2019

  MALINDI SC YALAZIMISHWA SARE YA 0-0 NA MOGADISHU CITY LEO KOMBE LA SHIRIKISHO

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  WAWAKILISHI wa Zanzibar kwenye Kombe la Shirikisho, Malindi SC nao wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Mogadishu City ya Somalia katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya kwanza jioni ya leo Uwanja wa Amaan.
  Sasa Malindi watajaribu tena bahati yao katika mchezo wa marudiano utakaofanyika Zanzibar pia wiki ijayo kwa ombi la wageni na mshindi atakutana na mwakilishi wa Misri.
  Matokeo hayo yanakuja siku moja baada ya jana, KMKM SC kuchapwa 2-0 na Primiero de Agosto ya Angola katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya kwanza Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Amaan.
  Timu hizo zitarudiana wiki ijayo mjini Luanda na mshindi wa jumla atakutana na mshindi kati ya Green Eagles FC ya Zambia na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MALINDI SC YALAZIMISHWA SARE YA 0-0 NA MOGADISHU CITY LEO KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top