• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 28, 2019

  YANGA SC YAANZA VIBAYA LIGI KUU, YACHAPWA BAO 1-0 NA RUVU SHOOTING LEO UHURU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Ruvu Shooting imeanza vyema msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwaangusha vigogo, Yanga SC kwa kuwachapa 1-0 jioni ya leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  Bao pekee la ushindi la Ruvu Shooting leo limefungwa na Saadat Mohammed dakika ya 20 aliyefanikiwa kuwazidi mbio mabeki wa Yanga kufuatia pasi ndefu ya mshambuliaji mwenza, Said Dilunga.
  Na bao hilo lilikuja baada ya Yanga kuanza vizuri mchezo na kupoteza nafasi nzuri ya kupata bao dakika ya kwanza tu kufuatia nyota wake, Mnamibia Sadney Urikhob kuunganishia juu ya lango krosi ya mshambuliaji mwenzake mpya, Mganda Juma Balinya.


  Lakini Yanga SC iliendele kupeleka mipira mbele kwenye eneo la Ruvu Shooting kusaka bao la kusawazisha, tatizo hawakuwa na maarifa ya kuipenya ngome ya wapinzani. 
  Nafasi nyingine nzuri na ya mwisho walitengeneza Yanga ilikuwa ni dakika ya 70 wakati mpira uliounganishwa kwa Nahodha na kiungo Papy Kabamba Tshishimbi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kufuatia krosi Ally Sonso kupangualiwa  na kipa Bidii Hussein.
  Mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu utahitimshwa kesho kwa mchezo kati ya mabingwa watetezi, Simba SC dhidi ya JKT Tanzania hapo hapo Uwanja wa Uhuru.
  Mechi nyingine za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, Lipuli iliirarua 3-1 Mtibwa Sugar, Azam FC iliichapa 1-0 Azam, Namungo ilishinda 2-1 dhidi ya Ndanda FC, Polisi Tanzania iliichapa 1-0 Coastal Union, Kagera Sugar ilishinda 2-0 ugenini dhidi ya Biashara United, Mwadui iliilaza 1-0 Singida United na Mbao ilitoa sare ya 1-1 na Alliance na Mbeya City ikatoka 0-0 na Tanzania Prisons.
  Kikosi cha Yanga SC kilikuwa: Farouk Shikalo, Mustafa Suleiman, Ally Mtoni ‘Sonso’, Lamine Moro, Papy Tshishimbi, Juma Balinya/Mapinduzi Balama dk53, Feisal Salum, Sadney Urikhob/Maybin Kalengo dk62 na Patrick Sibomana/Mrisho Ngassa dk69.
  Ruvu Shooting: Bidii Hussein, Omary Ally, Kassim Simbaulanga, Santos Mazengo, Rajab Zahir, Baraka Mtuwi, Edward Christopher/Abdul-Raham Mussa dk53, Shaaban Msala, Said Dilunga, Saadat Mohammed/Moses Shaaban dk71 na Emmanuel Martin/William Patrick dk77.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YAANZA VIBAYA LIGI KUU, YACHAPWA BAO 1-0 NA RUVU SHOOTING LEO UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top