• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 20, 2019

  KINACHOWEZA KUISAIDIA YANGA KUITOA TOWNSHIP ROLLERS KWAO

  Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Yanga SC Itashuka dimbani Agosti 24 JUMAMOSI ya wiki hii majira ya saa 10:00 za jioni kumenyana na wenyeji, Township Rollers katika mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Ikumbukwe kuwa mechi ya kwanza Yanga walitoa sare ya 1-1, na sasa Yanga watakuwa ugenini kutafuta mshindi wa jumla ili kusonga mbele, Yanga watalazimika kushinda mechi hiyo au sare ya goli kuanzia Goli 2 ili wasonge mbele lasivyo watakuwa wameyaaga mashindano.
  MAMBO MATANO YATAKAYOIBEBA YANGA.

  1: HISTORIA YA YANGA KWA MECHI ZA UGENINI
  Klabu ya Yanga imekuwa na historia nzuri na timu za kusini mwa Afrika ya kupata ushindi ugenini, mfano mzuri ni Komorozine ya Comoro, pamoja na BDF XI ya Botswana, hii endapo kama Yanga watajengwa vizuri kisaikolojia huenda ikawasaidia.
  .
  2: KUIMARIKA KWA BEKI YAO.
  Kelvin Yondani ameonekana kuleta kitu katika safu ya ulinzi ya Yanga mara baada ya kuungana na kambi hiyo safu ya ulinzi ya Yanga sasa na baadaye huenda ikawa tishio,lakini pia kurudishwa pembeni kwa Ally Mtoni Sonso kumeongeza ugumu wa safu ya ulinzi na kufanya viungo mda mwinyi kufikiria kutengeneza mashambulizi ingawa maelewano hasa sehemu ya mwisho sio mazuri kwani mikimbio ya washambuliaji inakuwa tofauti na mipira inayoletwa kupitia kati ya kiwanja ambapo kwa namna ya uchezaji wa Rollers ndio sehemu rahisi kupitika na kupata matokeo,pia maelewano ni mazuri kwa  Lamine Moro pamoja na Boxer huenda washambuliaji wa Rollers wakapata tabu sana katika kuipenya ngome ya *Yanga SC lakini umakini unatakiwa sana kwa kipa Metacha Mnata ambaye mechi ya awali alionesha kushindwa kujiamini baada ya Yanga kuruhusu bao la mapema.
  .
  3: MABADILIKO YA KIMFUMO.
  Yanga watalazimika kutumia mfumo utakao wasaidia wao kutengeneza nafasi nyingi za magoli kwa kuwatumia viungo wao hasa mfumo wa 4-2-3-1 wakiwa na mpira na mfumo wa 4-5-1 wakiwa hawana mpira ili kuweka uwiano katika maeneo yote matatu ya kiwanja ,kwa kuwatumia beki zao za pembeni na wenye kasi sana ,Yanga watalazimika kuwa na kasi mda wote kama wataitaji kushinda mchezo huo lasivyo wataumia ,washambuliaji Juma Balinya, Urikhob Sadney, Patrick Sibomana watahitajika kuwa makini zaidi pindi tu wafikapo langoni mwa timu pinzani na kutumia pasi za mwisho na krosi zitakazo kuwa zikichezwa.
  .
  4: GOLI LA MAPEMA ZAIDI.
  Kama wakitaka kuwachanganya zaidi wapinzani wao lazima Yanga wapate bao la mapema kabisa la sivyo watapa presha kubwa wakati mwingi wa mchezo ,naamini timu yoyote inapopata goli la mapema mpinzani wako hupoteana kabisa.
  .
  5: KUCHEZA BILA PRESHA YA MASHABIKI.
  Yanga huenda wakacheza soka safi la bila presha ya mashabiki wao wenye uchu na mafanikio kwa kuiona timu yao ikifanya vyema licha yakuwa watapata wakati mgumu sana kwa mashabiki wa rollers kwa kuzomewa ila hawatakosa mashabiki pia kwani msafara wa mamba na kenge wamo.

  TAHADHARI KWA YANGA:
  Washambuliaji wa Rollers Ni hatari zaidi wanapokuwa nyumbani hadi Sasa ligi ya mabingwa Afrika wamepachika goli zaidi ya 8 katika uwanja wao.
  YOTE KWA YOTE MECHI NI NGUMU SANA LAKINI MATOKEO KWA YANGA NI MUHIMU ZAIDINawapa Yanga 50% kushinda huu mtanange.

  (Dominick Salamba ni mchambuzi wa soka anapatikana pia kupitia katika Akaunti yake ya  Instagram kama @dominicksalamba au namba ya simu +255713942770)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KINACHOWEZA KUISAIDIA YANGA KUITOA TOWNSHIP ROLLERS KWAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top