• HABARI MPYA

  Jumapili, Agosti 11, 2019

  AZAM FC YACHAPWA 1-0 NA FASIL KENEMA MECHI YA KWANZA KOMBE LA SHIRIKISHO ETHIOPIA

  Na Mwandishi Wetu, BAHIR DAR
  TIMU ya Azam FC imeanza vibaya michuano ya Afrika baada ya kuchapwa 1-0 na wenyeji, Fasil Kenema katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya kwanza Kombe la Shirikisho Afrika mjini Bahir Dar, Ethiopia. 
  Azam FC inakuwa timu pekee ya Tanzania Bara kupoteza mechi ya kwanza ya michuano ya Afrika, baada y azote KMC, Simba na Yanga SC kutoa sare kwenye mechi zao za jana.
  Yanga ililazimishwa sare ya 1-1 na Township Rollers ya Botswana Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam na Simba SC ikatoka sare ya 0-0 na wenyeji, UD Songo mjini Beira, Msumbiji katika mechi za kwanza za raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa.

  Nayo KMC ikafanikiwa kupata sare ya ugenini ya 0-0 na wenyeji, AS Kigali katika katika mechi za kwanza za raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho na timu zote zitarudiana mwishoni mwa wiki ijayo.
  Azam FC na Fasil Kenema zitarudiana Agosti 24 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam na mshindi wa jumla atamenyana na mshindi kati ya Triangle FC ya Zimbabwe na Rukinzo FC ya Burundi, anapotokea kocha wao, Ettiene Ndayiragijje.
  KMC na AS Kigali zitarudiana wiki ijayo mjini Dar es Salaam mshindi wa jumla atakutana na mshindi kati ya Proline FC ya Uganda anapotokea kocha wao, Jackson Mayanja na Masters Security Services ya Malawi.
  Yanga na Rollers zitarudiana Jumamosi ijayo Uwanja wa Taifa mjini Gaborone, Botswana na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa mechi kati ya Green Mamba ya Eswatini na Zesco ya Zambia.
  Simba SC na UD Songo zitarudiana Jumapili ijayo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam na mshindi wa jumla atakutana na mshindi kati ya FC Platinum ya Zimbabwe na Nyasa Bullets ya Malawi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YACHAPWA 1-0 NA FASIL KENEMA MECHI YA KWANZA KOMBE LA SHIRIKISHO ETHIOPIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top