• HABARI MPYA

  Jumatatu, Agosti 12, 2019

  HISTORIA YA SOKA/KANDANDA/KABUMBU/MPIRA WA MIGUU.

  Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM
  UTANGULIZI: Mpira wa miguu au wengi wakipenda kuuita soka ,kandanda ,yote yakiwa ni majina sahihi ya mchezo huo.Soka ni nini? Soka ni mchezo unaochezwa na jumla ya wachezaji ishirini na wawili (22) katika timu mbili ikiwa na wachezaji kumi na mmoja kila timu na ndipo hukamilika 22.

  LENGO LA MCHEZO HUU NINI?
  Lengo la mchezo huu ni wachezaji kumiliki mpira kwa kutumia miguu na kufunga goli,yaani kuingiza mpira katika nyavu zilizosimamishwa na milingoti mitatu( kulia, Kushoto na juu.).Matumizi ya mikono ni marufuku isipokuwa tu kwa mlinda mlango au golikipa ndiye anayeruhusiwa kutumia mikono lakini na yeye ni katika sehemu yake maalumu tu sio kila sehemu,pia wakati wa kurudisha mpira baada ya kutoka nje mchezaji ataruhusiwa kutumia mikono kurudisha mpira ndani ya uwanja kwa kuurusha au kumrushia mchezaji mwenzake wa timu yake aliye ndani ya uwanja.
  Michezo mbalimbali ya kuchezea mpira inaweza kupatika katika maeneo mbalimbali ya kijiografia ,michezo mbalimbali ilianza kuchezwa muda mrefu ,Kipindi cha wagiriki ,waromania ambao walikuwa wakitumia michezo kwa ajili ya kuwaandaa wapiganaji kabla ya vita,kipindi cha nyuma na ndipo soka la kisasa lilianza nchini Uingereza.
  Kuibuliwa kwa mchezo huu wa mpira wa miguu (Soka) kulianzia wakati wa mashirikisho mawili (Shirikisho la mpira wa miguu na shirikisho la mpira wa Ragbi) yalipotawanyika ,ambapo basi shirikisho la kwanza la soka lilibaki nchini Uingereza.
  Mnamo mwaka 1963, Oktoba vilabu 2 vya london vilituma wawakilishi katika mkutano wa (Wajenzihuru) ili kujadili na kuweka kanuni zilizokubalika kusimamia mechi zilizochezwa kati yao,mkutano huo ulipelekea kuanzishwa kwa shirikisho la kandanda lililoitwa "Football Association",miongoni mwa kanuni zilizowekwa ni zile za kutaka utumiaji wa mikono kushika mpira na kunyang'anyana kwa mguu kama ilivyo kwa mchezo wa Ragbi, na hapo ndipo mwanzo wa Ragbi kugawanyika na mchezo wa soka.
  JE, UNATAKA KUJUA NINI KILIENDELA ,NI HAPA HAPA 
  (Dominick Salamba ni mchambuzi wa soka anapatikana pia kupitia Akaunti yake ya Instagram kupitia@dominicksalamba
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HISTORIA YA SOKA/KANDANDA/KABUMBU/MPIRA WA MIGUU. Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top