• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 20, 2019

  KIINGILIO CHA CHINI SIMBA SC NA UD SONGO NI SH 5,000 JUMAPILI UWANJA WA TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIINGILIO cha chini katika mchezo wa marudiano ya Raundi ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya wenyeji, SImba SC na UD Songo ya Msumbiji utakaofanyika Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni Sh. 5,000.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Sunday Manara alisema kwamba kiingilio hicho kitahusu majukwaa ya mzunguko, ambayo ndiyo hukusanya idadi kubwa zaidi ya watazamaji.
  Manara alisema viingilio vingine ni Sh. 15,000 kwa VIP B na C, Sh. 30,000 kwa VIP A. Sh. 100,000 kwa eneo la Platinums na 150,000 kwa Platinums Plus.

  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Manara akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam 

  Manara alisema kwamba kwa wenye kadi za Selcom wanaweza kuanza kununua tiketi mapema kupitia kwa mawakala, wakati tiketi za karatasi zitaanza kuuzwa Ijumaa.
  Kikosi cha Simba kinaendelea na maozezi yake Uwanja wa Gymkhana mjini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo huo, kikiwa kinahitaji ushindi wowote Jumapili baada ya sare ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza mjini Beira.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIINGILIO CHA CHINI SIMBA SC NA UD SONGO NI SH 5,000 JUMAPILI UWANJA WA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top