• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 31, 2019

  DULLAH MBABE ATWAA TAJI LA WBO BAADA YA KUMPIGA MCHINA KWA KO

  Na Mwandishi Wetu, QINGDAO 
  BONDIA Mtanzania, Abdallah Shaaban Pazi ‘Dullah Mbabe’ jana amefanikiwa kutwaa taji la WBO Asia Pacific uzito wa Middle baada ya kumpiga kwa Knockout (KO) raundi ya tatu mwenyeji, Zulipikaer Maimaitiali ukumbi wa TSSG Center mjini Qingdao, China.
  Dullah Mbabe alilianza pambano kwa kasi na kumpelekea makundi mfululizo Zulipikaer, bondia namba moja China ambaye ndiye aliyekuwa anashikilia mkanda huo, kabla ya kumkalisha chini raundi ya tatu. 
  Akizungumza baada ya pambano hilo, promota wa Dullah Mbabe, Jay Msangi amesema kwamba kijana wake ameliletea sifa taifa lake, Tanzania kwa ushindi huo.
  Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ (kushoto) akimuadhibu Zulipikaer Maimaitiali jana China

  “Ni heshima kubwa, wadau tujitokeze kwa wingi kwenye hafla ya kumpokea bingwa huyu siku ya Jumatatu saa tatu na nusu asubuhi pale uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Julias Nyerere,”alisema Jay Msangi.
  Kwa ushindi huo, sasa Dullah Mbabe anashikilia mataji mawili makubwa, lingine la WBF Intercontinental uzito wa Super Middle baada ya kumpiga Mtanzania mwenzake, Francis Cheka kwa KO pia raundi ya sita Desemba 26 mwaka jana ukumbi wa PTA. Saba Saba mjini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DULLAH MBABE ATWAA TAJI LA WBO BAADA YA KUMPIGA MCHINA KWA KO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top