• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 20, 2019

  INACHOHITAJI KUFANYA SIMBA SC KUWAMALIZA UD SONGO JUMAPILI

  Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Simba SC Jumapili itaingia Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kumenyana na UD Songo ya Msumbiji katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Baada ya sare ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza wa kwanza mjini Beira, Simba SC itahitaji ushindi wowote nyumbani ili kusonga mbele. Mambo yafuatayo yataibeba Simba.

  1: UWANJA WA NYUMBANI.
  Hakuna ubishi Simba SC  kwa sasa ndio inaongoza kujaza uwanja katika michuano ya kimataifa.Takribani mashabiki elfu 60 huingia uwanjani na kuwasapoti timu yao na hii ndio silaha kubwa kabisa kwa Simba kwa sasa,na ndiyo wanachojivunia,naamini siku ya Jumapili uwanja utajaa kama ilivyokuwa Simba Day na hilo Slsina shaka nalo.

  2: SAFU YA ULINZI IPUNGUZE MAKOSA.
  Mechi ya Ngao ya Jamii inaweza kuwa kipimo stahiki kabisa kwa Simba, makosa madogomadogo yaliyojitokeza kwenye safu ya ulinzi naimani mwalimu Patrick Aussems atakuwa ameona na kuyafanyia kazi, Erasto Nyoni ,Pascal Wawa wameonekana kuwa wazito sana katika kufanya maamuzi ya haraka,naamini kocha aliliona hilo.

  3: PATRICK AUSSEMS.
  Yeye ndiye atakayeamua hii mechi kulingana na aina ya wachezaji alionao,na mfumo upi autumie, naamini katika uwezo wake hilo sina shaka.

  4: MFUMO NA MIPANGO.
  Simba watalazimika zaidi kutumia 4-3-3  kwasababu ya kushambulia kwa  kasi ili kupata magoli mengi na kurudi kukaba kwa pamoja, Jonas Gerard Mkude,Mwamba wa Lusaka , Shiboub Sharaf ni  viungo bora kwa Sasa hilo halina ubishi,wengi wanamzungumzia Shiboub lakini Ni kwamba Jonas Mkude mimi naweza kusema ndio key player wa Simba anakaba,na kushambulia lakini kulingana na aina ya wachezaji alionaye naona amepunguziwa majukumuu kazi yake kubwa haswa Ni kukaba tu. Huku Chama na Shiboub wakienda kushambulia.
  Huku wengi wakimtaja Sharaf Shiboub, na kumsahau Jonasi Mkude kwa kazi anayoifanya kwa kufichwa na Sharaf ila Mkude ndio key players anayeamua amchezeshe nani je ampe Shiboub,je ampe Dilunga, je ampe Kanda. Hivyo mipira yote kabla ya kufika kwa Shiboub lazima ipite kwa Mkude na ndiyo iwafikie chama na wenzake.

  5: WASHAMBULIAJI WAONGEZE UMAKINI.

  Hakuna asiyemfahamu Kagere kwa uwezo wake ,ni mzoefu na anajua goli, hivyo winga zote ,viungo wanapaswa kumtafuta alipo na kumpigia mipira sehem sahihi alipo kagere. Ambapo atasaidiwa na Deo Kanda mzoefu pia na mechi za kitaifa, Hassani Dilunga Ni mtu mwenye kasi Sana, atawasumbua beki za Songo.

  6: MAGOLI YA MAPEMA
  Simba watalazimika kuingia uwanjani wakiwa na wazo moja tu,kufunga hicho ndio kitu cha msingi kwa wachezaji wa Simba, Ni lazima wapate goli ndani ya dakika 15 za kwanza ili kuwachanganya zaidi wapinzani wao na waanze kuzui mda wote hii itawasaidia Sana hata mbeki wa simba kujiamini na kupunguza makosa madogomadogo.

  ANGALIZO

  SIMBA WASIRUHUSU GOLI.

  UD Songo wao wataingia kwa kutafuta goli la ugenini hivyo watalazimika na wao kushambulia.


  YOTE KWA YOTE SIMBA INANAFASI KUBWA SANA YA KUSONGA MBELE, HII NI KWA SABABU YA WACHEZAJI WALIONAO, UZOEFU WALIOUPATA MSIMU ULIOPITA WAKIWA NDANI YA MASHINDANO HAYA. Nawapa 60% ya ushindi.
  (Dominick Salamba ni mchambuzi wa soka anapatikana pia kupitia katika Akaunti yake ya  Instagram kama @dominicksalamba au namba ya simu +255713942770)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: INACHOHITAJI KUFANYA SIMBA SC KUWAMALIZA UD SONGO JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top