• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 20, 2019

  KOCHA MICHO AWATEMA ORLANDO PIRATES, AJIUNGA NA ZAMALEK YA MISRI

  ALIYEWAHI kuwa kocha wa klabu ya Yanga, Mserbia Milutin ‘Micho’ Sredojević amejiunga na Zamalek ya Misri kufuatia kuachana ghafla na Orlando Pirates ya Afrika Kusini wiki hii.
  Baada ya kufanya kazi barani Afrika kwa takriban miongo miwili, Micho hapana shaka Micho ni miongoni mwa makocha wenye uzoefu mkubwa na michuano ya klabu ya barani Afrika. 
  Mserbia huyo alikuja barani Afrika mwaka 2001 na tangu amefundisha klabu za SC Villa ya Uganda, Saint George ya Ethiopia, Yanga SC ya Tanzania, Al Hilal ya Sudan na Orlando Pirates mata mbili.
  Mtihani wa kwanza wa Micho ambaye pia amefundisha kwa mafanikio timu za taifa za Rwanda na Uganda kwa vigogo wa Misri ni mchezo wa marudiano wa Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Dekedaha ya Somalia.
  Baada ya ushindi wa 7-0 kwenye mchezo wa kwanza mwishoni mwa wiki iliyopita Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria timu hizo zitarudiana hapo hapo wikie di hii kwa ombi la Wasomali hao.

  Kocha Mserbia Milutin ‘Micho’ Sredojević (wa pili kushoto) akisaini mkataba wa kujiunga na Zamalek nchini Misri baada ya kuachana Orlando Pirates 

  RATIBA MECHI ZA MARUDIANO LIGI YA MABINGWA
   IJUMAA AGOSTI 23, 2019
  Al Ahly (Misri) vs Atlabara (Sudan Kusini) (4-0)
  KCCA (Uganda) vs African Stars (Namibia) (2-3)
  Cote d’Or (Shelisheli) vs Fomboni (Comoro) (2-2)
  JUMAMOSI AGOSTI 24, 2019
  Raja Athletic Club (Morocco) vs Brikama United (Gambia) (3-3)
  El Merreikh (Sudan) vs JS Kabylie (Algeria) (0-1)
  Zamalek (Misri) vs Dekadaha (Somalia) (7-0)
  Generation Foot (Senegal) vs LPRC Oilers (Liberia) (0-1)
  Etoile du Sahel (Tunisia) vs Hafia (Guinea) (1-2)
  Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) vs AS Otoho (Kongo) (1-2)
  Zesco United (Zambia) vs Green Mamba (Eswatini) (2-0)
  Township Rollers (Botswana) vs Yanga SC (Tanzania) (1-1)
  FC Platinum (Zimbabwe) vs Big Bullets (Malawi) (0-0)
  Primeiro de Agosto (Angola) vs KMKM (Zanzibar) (2-0)
  Orlando Pirates (Afrika Kusini) vs Green Eagles (Zambia) (0-1)
  JUMAPILI AGOSTI 25, 2019
  El Nasr (Libya) vs Tempete Mocaf (Jamhuri ya Afrika Ya Kati) (0-1)
  Horoya (Guinea) vs Stade Malien (Mali) (1-1)
  ASCK (Togo) vs Buffles (Benin) (1-1)
  AS Vita (Cameroon) vs UMS de Loum (Cameroon) (0-0) 
  El Hilal (Sudan) vs Rayon Sports (Rwanda) (1-1)
  Enyimba (Nigeria) vs Rahimo (Burkina Faso) (0-1)
  USM Alger (Algeria) vs SONIDEP (Niger) (2-1)
  Gor Mahia (Kenya) vs Aigle Noir (Burundi) (0-0)
  Mekelle (Ethiopia) vs Cano Sport (Equatorial Guinea) (1-2)
  Asante Kotoko (Ghana) vs Kano Pillars (Nigeria) (2-3)
  Petro Atletico (Angola) vs Matlama (Lesotho)(2-0)
  Nouadhibou (Mauritania) vs SOA (Ivory Coast) (0-0)
  Elect Sport (Chad) vs CMS (Gabon) (0-0)
  Simba (Tanzania) vs UD Songo (0-0)
  Pamplemousses (Mauritius) vs Fosa Juniors (Madagascar (0-1)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KOCHA MICHO AWATEMA ORLANDO PIRATES, AJIUNGA NA ZAMALEK YA MISRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top