• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 29, 2019

  MAKAMU WA RAIS WA ZAMANI WA TFF, NASSIB AFARIKI DUNIA ATAZIKWA KESHO KISUTU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  ALIYEWAHI kuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ramadhani Nassib amefariki dunia alfajiri ya leo katika hospital ya Muhimbili mjini Dar es Salaam.
  Msiba huo umepkewa kwa majonzi makubwa na wadau mbalimbali wa michezo nchini, akiwemo Rais wa TFF, Wallace Karia ambaye ametuma salamu za pole kwa familia ya marehemu.
  Kwa mujibu wa taarifa ya familia, mwili wa marehemu utahifadhiliwa kesho baada ya Sala ya ijumaa katika makaburi ya Kisutu baada ya kusaliwa msikiti wa Maamur, Upanga mjini Dar es Salaam. Mungu ampumzishe kwa amani. Amin.

  Makamu wa Rais wa zamani wa TFF, Ramadhani Nassib (kushoto) amefariki dunia alfajiri ya leo hospital ya Muhimbili
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAKAMU WA RAIS WA ZAMANI WA TFF, NASSIB AFARIKI DUNIA ATAZIKWA KESHO KISUTU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top