// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NEYMAR ASAINI MIAKA MITANO PSG, MSHAHARA PAUNI 500,000 KWA WIKI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NEYMAR ASAINI MIAKA MITANO PSG, MSHAHARA PAUNI 500,000 KWA WIKI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Thursday, August 03, 2017

  NEYMAR ASAINI MIAKA MITANO PSG, MSHAHARA PAUNI 500,000 KWA WIKI

  HATIMAYE Neymar amekamilisha uhamisho wake wa rekodi ya dunia wa Pauni Milioni 198 kwenda Paris Saint-Germain kutoka Barcelona. 
  Baada ya wiki kadhaa za tetesi kuhusu dili hilo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amesaini mkataba wa miaka mitano ambao atakuwa analipwa Pauni 500,000 kwa wiki na klabu hiyo ya Ufaransa na anatarajiwa kuichezea mechi ya kwanza Agosti 5 nyumbani kwa Amiens katika Ligue 1. 
  Neymar, ambaye atatambulishwa rasmi Ijumaa mchana, amesema: "Tangu nimewasili Ulaya, klabu hiyo imekuwa moja ya washindani wakubwa na yenye matarajio zaidi.


  Neymar amesaini mkataba wa miaka mitano kujiunga na Paris Saint-Germain kutoka Barcelona
   
  PICHA ZAIDI GONGA HAPA


  "Na changamoto kubwa, ambacho kinanivutia zaidi mimi kuungana na wachezaji wenzangu wapya ni kuisaidia klabu kutwaa mataji ambayo mashabiki wake sanataka. Matarajio ya Paris Saint-Germain yamenivutia mimi katika klabu, pamoja na shauku na nguvu iliyowekwa,". 
  "NImecheza misimu minne Ulaya na ninahisi nipo tayari kuchukua changamoto hiyo. Kutokaa leo, nitafanya kitu chochote nitakachoweza kuwasaidia wachezaji wenzangu wapya, kufungua usawa mpya kwa klabu yangu na kuwapa furaha mamilioni ya mashabiki wake duniani," amesema Neymar. 
  Kwa upande wake, Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi amesema: "Ni kwa furaha kubwa na tunamkaribisha Neymar hapa Paris Saint-Germain. "Mawazo yake ya ushindi, nguvu ya tabia yake na hisia za kiuongozi vimemfanya awe mchezaji mkubwa,". 
  Rais huyo ameonyesha matumaini makubwa ya kufanya vizuri zaidi katika ulimwengu wa soka baada ya kumpata mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil.
  Lakini wazi kuondoka kwa Neymar ni pigo Barcelona, kwani safu yao kali ya ushambuliaji iliyokuwa inaundwa na mapacha watatu, pamoja na Lionel Messi na Luis Suarez ikijulikana kama MSN imebomoka.
  Na sasa Barca inahusishwa mno na mpango wa kumchukua mshambuliaji mwingine Mbrazil, Philippe Coutinho kutoka Liverpool huo ukiwa mpango wa kocha mpya, Ernesto Valverde kuziba pengo hilo Nou Camp.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NEYMAR ASAINI MIAKA MITANO PSG, MSHAHARA PAUNI 500,000 KWA WIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top