• HABARI MPYA

    Saturday, August 06, 2016

    MANJI AWAFUKUZA UANACHAMA YANGA MKEMI, NYENZI NA HASHIM

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MKUTANO Mkuu wa dharula wa Yanga SC umewafukuza wanachama watatu wa klabu hiyo, Ayoub Nyenzi, Salum Mkemi na Hashim Abdallah.
    Mwenyekiti Yussuf Manji aliwaambia wanachama hayuko tayari kufanya kazi na Wajumbe hao wa Kamati ya Utendaji na akaomba wanachama wanaowataka wajitokeze kupiga kura, lakini hakuna aliyeinuka.
    Baada ya kurudia kuita mara tatu, Hashim pekee kati ya watatu hao ambaye alikuwepo mkutanoni ukumbi wa Diamond Jubilee, akainuka na kuondoka.
    Hashim Abdallah akiondoka ukumbi wa mkutano leo Diamond Jubilee
    Hashim akiimaliza meza kuu wakati anaondoka 
    Hashim akiwaaga ndugu na jamaa mbalimbali wakati anaondoka
    Hashim aliondoka kwa furaha tu ukumbini

    Hashim Abdallah (kulia) wakati wa Mkutano leo Diamond Jubilee 
    Mwanachama mwingine, Siza Lyimo ambaye Manji alitaka aondoke, yeye aliomba msamaha na wanachama wakamsamehe na Mwenyekiti huyo akabariki msamaha huo.
    Mkemi na Nyenzi hawakutokea kwenye Mkutano huo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MANJI AWAFUKUZA UANACHAMA YANGA MKEMI, NYENZI NA HASHIM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top