• HABARI MPYA

  Jumatatu, Agosti 22, 2016

  BEKI ALIYEANGUKA CHOONI SIMBA ANAENDELEA VIZURI, ANAWEZA KURUHUSIWA SIKU MBILI HIZI

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  BEKI mpya wa Simba SC, Hamad Juma aliyeanguka bafuni mwishoni mwa wiki nyumbani kwake na kulazwa hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam, anaendelea vizuri.
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Sunday Manara ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba beki huyo wa kulia anaendelea vizuri baada ya matibabu ya takriban saa 24.
  “Anaendelea vema na ndani ya siku mbili kuanzia kesho anaweza kuruhusiwa kurudi nyumbani. Tunamshukuru Mungu,”amesema Manara. 
  Manara amesema mchezaji huyo aliyesajiliwa msimu huu kutoka Coastal Union ya Tanga, aliteleza bafuni na kufikia kichwa ambacho kilipasua kidogo.
  Hamad Juma (kushoto) katika mchezo dhidi ya Ndanda FC, hapa anamtoka Salum Telela
  “Baada ya kukimbizwa hospitali alifanyiwa uchunguzi wa kina na kisha kupatiwa tiba, ikiwemo kushonwa nyuzi kadhaa, ila hali yake inaendelea vema kwa sasa,”alisema Manara.
  Tayari Hamd Juma amefanikiwa kuwa beki chaguo la kwanza wa kulia wa Simba SC, mbele ya kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog baada ya kucheza vizuri mechi mbili zilizopita dhidi ya URA katika sare ya 1-1 na dhidi ya Ndanda FC katika ushindi wa 3-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Na kwa ajali hii, wazi Hamad atakosekana katika mchezo ujao dhidi ya JKT Ruvu Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BEKI ALIYEANGUKA CHOONI SIMBA ANAENDELEA VIZURI, ANAWEZA KURUHUSIWA SIKU MBILI HIZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top