• HABARI MPYA

  Jumatatu, Agosti 29, 2016

  MKWASA AMUITA STARS KIPA ALIYEIKATALIA SIMBA JUMAMOSI TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa, amefanya mabadiliko kwenye kikosi kinachotarajiwa kusafiri Jumatano Agosti 31, 2016 kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa kukamilisha ratiba ya kuwania tiketi ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) dhidi ya wenyeji, Nigeria.
  Mabadiliko yaliyofanyika ni kwa kumchukua Kipa kinda wa JKT Ruvu, Said Kipao kuchukua nafasi ya Deogratius Munishi 'Dida' ambaye amefiwa na jana.
  Kipao alimvutia Mkwasa baada ya kudaka vizuri Jumamosi kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara timu yake JKT Ruvu ikilazimisha sare ya 0-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Mussa Kipao alidaka vizuri Simba ikil;azimishwa sare na JKT Ruvu Jumamosi 
  Tayari Misri imefuzu kutoka kundi G ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo iliyojitoa katikati ya mashindano.
  Wachezaji wanaounda kikosi cha Stars ambacho kimeingia kambini Hoteli ya Urban Rose mjini Dar es Salaam ni makipa Said Kipao – JKT Ruvu, Aishi Manula – Azam FC, Mabeki; Kevin Yondani, Vicent Andrew, Mwinyi Hajji Mngwali (wote Yanga SC), Mohamed Hussein 'Tshabalala' (Simba SC), Shomari Kapombe na David Mwantika (wote Azam FC).
  Viungo ni Himid Mao (Azam FC), Shiza Kichuya (Simba SC), Ibrahim Jeba (Mtibwa Sugar), Jonas Mkude (Simba SC), Muzamil Yassin (Simba SC), Juma Mahadhi (Yanga SC) na Farid Mussa (Tenerif, Hispania)
  Washambuliaji ni Simon Msuva (Yanga SC), Jamal Mnyate, Ibrahim Ajib (Simba SC), John Bocco (Azam FC) na 
  Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MKWASA AMUITA STARS KIPA ALIYEIKATALIA SIMBA JUMAMOSI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top