• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 30, 2016

  SIMBA SC YATAKIWA KUILIPA MAMILIONI COASTAL UNION

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji imeitaka klabu ya Simba SC kuilipa Coastal Union fidia ya Sh. Milioni 5 kutokana na usajili wa wachezaji Ibrahim Shekwe, Hemed Hamisi na Abdi Banda. 
  TFF pia imeridhia kocha Mganda Ametre Richard kumalizana na Simba SC juu ya madai yao ya malimbikizo ya mishahara. 
  Kamati imeridhia pande mbili kwenda kulimaliza suala hilo nje ya kamati kama ambavyo wameomba. Wamekubaliana kukutana Jumatano Agosti 31, 2016 na kuleta yatokanayo TFF.
  Rais wa Simba SC, Evans Aveva ambaye klabu yake imetakiwa kuilipa Coastal Union

  Aidha, malalamiko ya mchezaji Ally Rashid Ally kudai kunyimwa stahiki zake na Klabu ya Simba. Shauri hili sasa litasikilizwa Jumapili ijayo ya Septemba 4, 2016 baada ya kushindikana kusikilizwa kutokana na mdai Ally Rashid Ally kutotokea kwenye kesi. Ally Rashid Ally ameagizwa kukuhudhuria shauri hilo, vinginevyo litasikilizwa upande mmoja na kutolewa uamuzi upande mmoja.
  Katika mashauri mengine, malalamiko ya Kocha Mathias Lule. Lule anadai mshahara, usajili na bima ya matibabu kwa Stand United. Kamati imeridhia pande mbili kwenda kulimaliza suala hilo nje ya kamati kama ambavyo wameomba. Wamepewa wiki moja kufanya hivyo na na kuleta yatokanayo TFF.
  Kamati umeamua kuwa Mbeya City ya Mbeya iwalipe wachezaji wake wa zamani, Abdallah Juma, Temi Felix na Erick Mawala madai yote ya malimbikizo ya mshahara na fedha za usajili.
  Kinondoni Sports Academy (KISA) inadai fidia za malezi kwa Azam baada ya kumsajili mchezaji Omary Maunda, ambako Kamati imeridhia pande mbili kwenda kulimaliza suala hilo nje ya kamati kama ambavyo wameomba. Wamepewa wiki moja kufanya hivyo na na kuleta yatokanayo TFF.
  KISA inadai fidia za malezi kwa Kagera Sugar baada ya kumsajili mchezaji Hussein Abdallah, ambako Kamati imeridhia pande mbili kwenda kulimaliza suala hilo nje ya kamati kama ambavyo wameomba. Wamepewa wiki moja kufanya hivyo na na kuleta yatokanayo TFF.
  KISA inadai fidia za malezi kwa Mtibwa Sugar baada ya kumsajili mchezaji Daniel Jemedari, ambako Kamati imeridhia pande mbili kwenda kulimaliza suala hilo nje ya kamati kama ambavyo wameomba. Wamepewa wiki moja kufanya hivyo na na kuleta yatokanayo TFF.
  KISA inadai fidia za malezi kwa Majimaji ya Songea baada ya kumsajili mchezaji Joseph Njovu. Shauri hili sasa litasikilizwa Jumapili ijayo ya Septemba 4, 2016 baada ya kushindikana kusikilizwa kutokana na mdaiwa Majimaji kutotokea kwenye kesi. Majimaji wameagizwa kukuhudhuria shauri hilo vinginevyo litasikilizwa upande mmoja na kutolewa uamuzi upande mmoja.
  KISA inadai fidia za malezi kwa Toto African ya Mwanza baada ya kumsajili mchezaji Jafari M. Jafari, ambako Kamati imeridhia pande mbili kwenda kulimaliza suala hilo nje ya kamati kama ambavyo wameomba. Wamepewa wiki moja kufanya hivyo na na kuleta yatokanayo TFF.
  KISA inadai fidia za malezi kwa JKT Ruvu ya Pwani baada ya kumsajili mchezaji Najimu Maguru, ambako Kamati imeridhia pande mbili kwenda kulimaliza suala hilo nje ya kamati kama ambavyo wameomba. Wamepewa wiki moja kufanya hivyo na na kuleta yatokanayo TFF.
  Coastal Union ilileta malalamiko dhidi ya Kagera Sugar kuhusu madai ya fidia ya mchezaji Ibrahim Sheku. Kamati imeridhia pande mbili kwenda kulimaliza suala hilo nje ya kamati kama ambavyo wameomba. Wamepewa wiki moja kufanya hivyo na na kuleta yatokanayo TFF.
  Coastal Union ilileta malalamiko dhidi ya Mbeya City kuhusu madai ya fidia ya wachezaji Fikirini Bakari na Ayub Yahaya. Kamati imeridhia pande mbili kwenda kulimaliza suala hilo nje ya kamati kama ambavyo wameomba. Wamepewa wiki moja kufanya hivyo na na kuleta yatokanayo TFF.
  Coastal Union ilileta malalamiko dhidi ya JKT Ruvu kuhusu madai ya fidia ya mchezaji Yusuf Chuma. Shauri hili sasa litasikilizwa Jumapili ijayo ya Septemba 4, 2016 baada ya kushindikana kusikilizwa kutokana na mdaiwa JKT Ruvu kutotokea kwenye kesi. JKT Ruvu wameagizwa kukuhudhuria shauri hilo vinginevyo litasikilizwa upande mmoja na kutolewa uamuzi upande mmoja.
  Malalamiko ya Kocha Bakari Shime kudai ya mshahara dhidi ya Mgambo JKT. Kamati umeamua kuwa Mgambo JKT imlipe Shime na uongozi wa klabu hiyo umeahidi kumlipa Shime kiasi cha Sh 8,500,000 ndani ya wiki tatu kuanzia tarehe ya uamuzi huu.
  Malalamiko ya wachezaji Wachezaji Omary Seseme, Said Omary na Edward Christopher dhidi ya Toto African kudai mishahara na fedha za usajili. Kamati umeamua kuwa Toto African iwalipe wachezaji hao na uongozi wa klabu hiyo umeahidi kumlipa ndani ya wiki mbili kuanzia tarehe ya uamuzi huu.
  Malalamiko ya wachezaji Rajab Isihaka na Said Mketo v Ndanda FC dhidi ya Ndanda kudai mishahara na fedha za usajili. Kamati imeridhia pande mbili kwenda kulimaliza suala hilo nje ya kamati kama ambavyo wameomba. Wamepewa wiki moja kufanya hivyo na na kuleta yatokanayo TFF.
  Lipuli ilileta malalamiko dhidi ya Mbeya City kumsajili mchezaji Mackyada Makolo bila kufuata utaratibu. Shauri hili sasa litasikilizwa Jumapili ijayo ya Septemba 4, 2016 baada ya kushindikana kusikilizwa kutokana na mdaiwa Mbeya City kutotokea kwenye kesi. Mbeya City wameagizwa kukuhudhuria shauri hilo vinginevyo litasikilizwa upande mmoja na kutolewa uamuzi upande mmoja.
  Lipuli ilileta malalamiko dhidi ya JKT Ruvu kumsajili Mchezaji Kassim Kisengo bila kufuata utaratibu ikiwa ni pamoja na kutolipa ada ya mkoa na wilaya. Pande zote mbili zilimalizana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YATAKIWA KUILIPA MAMILIONI COASTAL UNION Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top