• HABARI MPYA

  Jumapili, Agosti 28, 2016

  DIDA AFIWA NA BABA, KASEKE AFIWA NA BABU

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  WACHEZAJI wawili wa Yanga SC, kipa Deo Munishi ‘Dida’ na kiungo Deus Kaseke walipokea habari za kuhuzunisha baada ya mchezo dhidi ya African Lyon leo.
  Mara baada ya kuiwezesha Yanga kuanza vyema mbio za kutetea taji la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya African Lyon Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wawili hao wakapewa taarifa za msiba.
  Dida aliyedaka vizuri leo amefiwa na baba yake mzazi wakati Kaseke aliyecheza vizuri amefiwa na babu yake.  
  Dida amepokea habari za kuhuzunisha baada ya kulinda vizuri lango la Yanga ikishinda 3-0

  Dida alilinda lango la Yanga vizuri bila kuruhusu nyavu kutikiswa na Kaseke akafungua biashara nzuri kipindi cha kwanza kwa bao la kwanza, kabla ya Simon Msuva na Juma Mahadhi kufunga mengine kipindi cha pili.
  Msiba wa Dida upo Mikoroshini Temeke, wakati msiba wa Kaseke upo Mbeya. Yanga itashuka tena dimbani Jumatano kumenyana na JKT Ruvu katika mfululizo wa Ligi Kuu na uwezekano wa wawili hao kucheza ni mdogo sasa. 
  Dida (kushoto) akiwa na baba yake (katikati) hospitali kabla ya kufikwa na umauti 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DIDA AFIWA NA BABA, KASEKE AFIWA NA BABU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top