• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 27, 2016

  SIMBA SC YABANWA NA JKT RUVU, SARE 0-0 TAIFA

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imelazimishwa sare ya bila kufungana na JKT Ruvu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
  Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Selemani Kinugani wa Morogoro, aliyesaidiwa na Josephat Bulali wa Tanga na Omar Juma wa Dodoma, timu zote zilishambuliana kwa zamu.
  Dakika ya saba mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Frederick Blagnon alipewa pasi nzuri na kiungo Jamal Mnyate, lakini shuti lake likadakwa na kipa wa JKT, Said Kipao.
  Dakika ya 19 winga wa Simba Shizza Kichuya alipiga shuti kali na Kipao akapangua kabla ya JKT kujibu dakika ya 18 baada ya shuti kali la Saad Kipanga kufuatia pasi ya Atupele Green na kipa Vincent Angban.
  Mshambuliaji Mrundi wa Simba, Laudit Mavugo akitafuta maarifa ya kumpita beki wa JKT Ruvu, Rahim Juma 
  Mshambuliaji wa Simba, Muivory Coast Frederic Blagnon akimtoka beki wa JKT Ruvu, Pera Mavuo
  Winga wa Simba SC, Shizza Kichuya akimtoka beki wa JKT Ruvu, Rahim Juma 

  Simba SC ilipata pigo dakika ya 73, baada ya beki wake Novat Lufunga kuumia mkono na nafasi yake kuchukuliwa na Juuko Murshid. 
  Kuingia kwa Mwinyi Kazimoto aliyechukua nafasi ya Jamal Mnyate na Ibrahim Hajib aliyechukua nafasi ya Blagnon kuliongeza kasi ya mashambulizi ya Simba, lakini sifa zimuendee kipa Said Kipao aliyeokoa michomo kadhaa ya hatari.
  Kwa matokeo hayo, Simba inaangukia nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake nne, sawa na Azam FC wanaoongoza kwa wastani mzuri wa mabao.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Azam FC  imeshinda 3-0 dhidi ya Majimaji ya Songea Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam mabao ya Shomary Kapombe, Mudathir Yahya na Nahodha John Bocco.
  Mtibwa Sugar imepata ushindi wa kwanza baada ya kuilaza 2-0 Ndanda FC Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro, wakati Mwadui FC imeshinda 1-0 dhidi ya wenyeji Mbao FC Uwanja wa Kirumba, Mwanza, Prisons imelazimishwa sare ya 1-1 na Ruvu Shooting sawa na Stand United iliyotoka 0-0 na Kagera Sugar.
  Kikosi cha Ruvu Shooting kilikuwa; Said Kipao, Michael Aidan/James Msuva dk23/Nashon Naftali dk46, Salim Gilla, Murdin Mohammed, Rahim Juma, Ismail Amour, Hassan Matelema, Hassan Dilunga, Atupele Green, Saad Kipanga na Pera Mavuo.
  Simba SC; Angban, Malika Ndeule, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novat Lufunga/Juuko Murshid dk73, Method Mwanjali, Jamal Mnyate/Mwinyi Kazimoto dk51, Jonas Mkude, Frederick Blagnon/Ibrahim Hajib dk60, Shizza Kichuya, Laudit Mavugo na Muzamil Yassin. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YABANWA NA JKT RUVU, SARE 0-0 TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top