• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 30, 2016

  SIMBA WAENDA KUPASHA KIAINA DOM

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Simba inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Polisi Dodoma Ijumaa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
  Msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara, amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba mchezo huo umetokana na mamombi uya Chama cha soka mkoani humo ambao wameiomba klabu hiyo kwenda kucheza mchezo wa kirafiki ili kuinua molali ya soka.
  Manara, alisema timu hiyo itaondoka kesho kuelekea Dodoma tayari kwa ajili ya mchezo huo.
  "Kama unavyojua kwetu michezo ya ligi imesimama kutokana na majukumu ya timu ya taifa ambayo inawachezaji wetu sita,tumeona ni vyema basi kulifanyia kazi ombi la wenzetu wa Dodoma," alisema Manara.
  Alisema mchezo huo utakuwa sehemu ya maandalizi kwa kocha Joseph Omog kuelekea kwenye mechi yao ijayo ya ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting.
  Mchezo uliopita wa ligi, Simba ilibanwa mbavu na JKT Ruvu na kutoka suluhu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA WAENDA KUPASHA KIAINA DOM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top