• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 26, 2016

  TANZANIA YAPIGWA ‘WIKI’ NA IVORY COAST SOKA LA UFUKWENI

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  TANZANIA imefungwa mabao 7-3 na Ivory Coast katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika soka la Ufukweni baadaye mwaka huu Lagos.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wageni walianza vizuri na kufanikiwa kuongoza kwa mabao 2-1 hadi mwisho wa robo ya kwanza.
  Lakini wenyeji wakajitutumua na kumaliza robo ya pili wakiwa wamefungana mabao 3-3.
  Mchezaji wa Tanzania, Samuel Sarungi (kushoto) akimtoka mchezaji wa Ivory Coast, Kouassitch Daniel leo Uwanja wa Karume
  Rolland Revocatus Kessy (kushoto) akipiga kichwa mbele ya Djere Fabien Sola 

  Hata hivyo, mambo yakawa magumu upande wa wenyeji kuanzia robo ya tatu na kujikuta wanamaliza mchezo wakiwa wameloa 7-3.
  Mabao ya Ivory Coast yamefungwa na Kablan Assouan Bile matano na Aka Kablan  Frederick mawili, wakati ya Tanzania yamefungwa na Ally Rabi Abdallah mawili na Kashiru Salum Said.
  Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Ally Rabby Abdallah, Rajab Ghana Kipango, Roland Revocatus Kessy, Juma Sultan Ibrahim, Ahmada Abdi Ahmada.
  Wlioanzia benchi; Ahmed Rajab Juma, Yakoub Mohammed Nassor, Samuel Sarungin Opanga, Kashiru Salum Said na Mohamed Makame Silima
  Ivory Coast; Djedjed Guy Hans, Kouassitch Daniel, Aka Kablan Frederick, Kouadio Brou Armand na Kablan Assouan Bile.
  Walioanzia benchi; Aidara Mory, Djere Fabien Sola, Eric Tchetche, Didier Kebletchi, Zemene Gnoleba, Soro Kingman na Badi Anouma.    
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TANZANIA YAPIGWA ‘WIKI’ NA IVORY COAST SOKA LA UFUKWENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top