• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 25, 2016

  MSIMU MPYA WA LIGI KUU YA VODACOM 2016/2017 WAANZA KWA MSISIMKO

  LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara VPL ilifunguliwa rasmi wikiendi iliyopita kwa mechi 6 kuchezwa katika viwanja tofauti. Katika mechi ya Simba dhidi ya Ndanda FC tulishuhudia Simba ikipata ushindi wa magoli 3 – 1 huku winga mpya wa Simba, Shiza Kichuya akifanikiwa kufunga bao zuri kuhitimisha karamu ya magoli 3.
  Kule Morogoro, Mtibwa Sugar wakiwa uwanja wa nyumbani waliduwazwa na Ruvu Shooting baada ya kupokea kichapo ch goli moja bila. Akizungumza siku moja baada ya mechi hiyo Kocha wa Mtibwa Sugar Salum Mayanga alisema kipigo hicho kimewazindua usingizini hivyo wanajipand zaidi kwa mechi zijazo.


  Azam FC ilinusurika kupokea kipigo kutoka kwa African Lyon ambapo John Bocoo aliisawazishia timu hiyo katika dakika za majeruhi. Katika mchezo huo African Lyon walionekana kucheza kandanda safi, “hii timu inacheza kana kwamba ilikuwa inacheza ligi kuu kwa muda mrefu sana, itasumbua kweli kweli” alisikika mmoja wa watazamaji akifuatilia mechi hiyo kupitia “Kibanda Umiza” maeneo ya Kijitonyama. Nae kocha mkuu wa klabu ya Azam FC ambayo mwaka huu imefanikiwa kuchukua Ngao ya Jamii alisema kuwa anahitaji muda zaidi ili kukisuka kikosi chake na kucheza kupitia mifumo wanayoendelea kuwafundisha wachezaji wa timu hiyo. “Kwa sasa tunafanya tathmini ya mchezo uliopita, kutoa makosa na kurekebishana pale tulipokosea, tukimaliza hapo kwa wiki hii tutaanza kujipanga kwa mchezo ujao (Majimaji), lakini cha kwanza tunaangalia yali yaliyotokea katika mchezo wa kwanza, mapungufu yalikuwa wapi na nani anapaswa kufanya nini,” alisema.
  Mechi ya Stand United na Mbao FC timu iliyopanda daraja haikufanikiwa kutoa mshindi na kule Songea timu ya Majimaji ilikubali kupokea kichapo cha goli 1 – 0 kutoka kwa Tanzania Prisons. Hii leo kutakuwa na mchezo mmoja utakaochezwa jijini Mwanza ambapo Toto Africans itamenyana na Mwadui FC. Msimu uliopita mechi mbili za ugenini na nyumbani za timu hizi ziliisha kwa ushindi wa goli 1 bila huku kila timu ikitamba kwenye uwanja wake.
  Kwenye picha baadhi ya wafanyakazi kutoka Idara ya Masoko ya Vodacom Tanzania wakiongozwa na Mkuu wa Idara hiyo Nandi Mwiyombella (katikati) walifika kushuhudia mechi kati ya Simba na Ndanda.
  Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu uliopita hawakucheza mechi yao ya ufanguzi ili kupata nafasi ya kujiandaa na mechi ya Shirikisho dhidi ya TP Mazembe. Yanga itaanza kampeni ya msimu huu hapo Jumamosi kwa kucheza na African Lyon.
  Endele Kufuata kurasa zetu kwenye mitandao ya kijamii ukitumia #VPL2016 uweze kutabiri matokeo ya mechi na kupata taarifa zaidi kuhusu ligi kuu ya Vodacom. Pia kupata live match updates kila wiki.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MSIMU MPYA WA LIGI KUU YA VODACOM 2016/2017 WAANZA KWA MSISIMKO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top