• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 25, 2016

  MAZEMBE KUMENYANA NA ETOILE DU SAHEL NUSU FAINALI AFRIKA

  RATIBA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA
  Sept 16-18, 2016
  Zamalek (Misri) Vs Wydad Athletic Club (Morocco)
  Zesco (Zambia) Vs Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)
  RATIBA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO
  Sept 23-25, 2016
  TP Mazembe (DRC) Vs Etoile du Sahel (Tunisia)
  MO Bejaia (Algeria) Vs FUS Rabat (Morocco)
  TP Mazembe itamenyana na Etoile du Sahel ya Tunisia katika Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Afrika

  TIMU za Kusini mwa Afrika zitamenyana zenyewe kwa zenyewe katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kama itakavyokuwa kwa timu za Kaskazini mwa Bara kuelekea kwenye kinyang'anyiro cha dola za Kimarekani Milioni 1.5 na tiketi ya kucheza Klabu Bingwa ya Dunia nchini Japan.
  Mabingwa mara tano barani, Zamalek ya Misri watamenyana na vigogo wa Morocco, Wydad Athletic kuwania tiketi ya Fainali, wakati Zesco United ya Zambia itamenyana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
  Timu za Kusini mwa Afrika zimefuzu pasipo kutarajiwa hususan Zesco, ambayo ilikuwa kundi moja na mabingwa watatu wa zamani, Al Ahly ya Misri, ASEC Mimosas ya Ivory Coast na Wydad.
  Wakiwa wanakwenda Nusu Fainali kwa mara ya pili tu, Zesco inatarajiwa kuitoa Sundowns, iliyofungwa katika fainali miaka 15 iliyopita.
  Kwa Zamalek, hii inaakuwa mara ya kwanza kufika Nusu Fainali tangu mwaka 2005, wakati Wydad walifika hatua hiyo kwa mara ya mwisho mwaka 2011, kabla ya kufungwa na Esperance ya Tunisia kwenye fainali.
  Mechi za kwanza zinatarajiwa kuchezwa wikiendi ya Septemba 16 hadi 18, wakati marudiano yatakuwa wikiendi ya Septemba 23  na 25.
  Na katika Kombe la Shirikisho, TP Mazembe ya DRC itamenyana na Etoile du Sahel ya Tunisia wakati MO Bejaia ya Algeria itamenyana na FUS Rabat ya Morocco katika Nusu Fainali.
  Mechi za kwanza pia zinatarajiwa kuchezwa wikiendi ya Septemba 16 hadi 18, wakati marudiano yatakuwa wikiendi ya Septemba 23  na 25.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAZEMBE KUMENYANA NA ETOILE DU SAHEL NUSU FAINALI AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top