• HABARI MPYA

  Jumatatu, Agosti 29, 2016

  KIPA NAMBA 1 CHELSEA AJIONEA MWENYEWE SHUGHULI LA SAMATTA AKAMUAMBIE CONTE

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  KIPA namba moja wa Chelsea, Thibaut Nicolas Marc Courtois jana alimshuhudia vizuri mshambuliaji wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
  Na hiyo ilitokea siku moja baada ya Mbelgiji huyo kukiongoza kikosi cha Mtaliano, Antonio Conte kushinda 3-0 Uwanja wa Stamford Bridge, London katika mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Burnley Jumamosi.    
  Courtois alikuwepo jana Luminus Arena, KRC Genk ikishinda 1-0, bao pekee la Alejandro Pozuelo dakika ya 79 katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A ya Ubelgiji.
  Courtois alikuwepo jana Luminus Arena, KRC Genk ikishinda 1-0,
  Mbwana Samatta akipambana jana Uwanja wa Luminus Arena, KRC Genk ikishinda 1-0

  Kipa huyo mrefu mzaliwa wa Bree, Courtois kisoka alianzia Bilzen V.V. ya kwao kama beki wa kushoto, lakini hakudumu sana hapo akaenda Genk mwaka 1999 akiwa na umri wa miaka saba tu na ni huko alikobadilishwa na kuwa kipa.
  Akiwa na umri wa miaka 16 na siku 341 Genk msimu wa 2010–2011 baada ya kuibuka kupitia mfumo wa vijana, Courtois akachezea mechi yake ya kwanza kikosi cha kwanza cha Genk Aprili 17 mwaka 2009 dhidi ya Gent. 
  Akatoa mchango mkubwa kwa timu hiyo kutwaa taji la Ligi Kuu ya Ubelgiji msimu wa 2010–2011 kabla ya kushinda tuzo ya Kipa Bora wa Mwaka na Mchezaji Bora wa Mwaka wa Genk, kwa kufungwa mabao 32 tu katika mechi 40 za ligi na kudaka mechi 14 bila kuruhusu nyavu zake kuguswa.
  Courtois jana alimshuhudia vizuri Mbwana Ally Samatta Uwanja wa Luminus Arena 
  Samatta alicheaa vizuri jana Uwanja wa Luminus Arena japokuwa hakufunga

  Na imekuwa kawaida kutembelea klabu iliyomuibua kisoka na jana alikuwepo kwa mara ya kwanza tangu Samatta asajiliwe Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC.
  Katika mchezo wa jana, kikosi cha Genk kilikuwa; Bizot, Walsh, Dewaest, Colley, Uronen, Heynen/Karelis dk69, Ndidi, Pozuelo, Trossard/Nastic dk76, Buffalo na Samatta.
  Zulte-Waregem: Bossut, the Fauw, Baudry, Derijck, Lerager/Vetokele dk82, Leye, Kaya, Meite, Lepoint/Oulare dk88, Cordaro/Koopmans dk80 na Hamalainen.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIPA NAMBA 1 CHELSEA AJIONEA MWENYEWE SHUGHULI LA SAMATTA AKAMUAMBIE CONTE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top