• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 26, 2016

  KOCHA MRENO WA AFRICAN LYON AMFUKUZA BEKI WA SIMBA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mreno wa African Lyon, Fernando Jose Bernado Tavares amemfukuza beki Mohamed Fakhi aliyesajiliwa kutoka Simba SC kwa utovu wa nidhamu.
  Tavares inadaiwa alikerwa na tabia za kuchelewa mazoezini za Fakhi na akasema hamuhitaji tena katika kikosi chake.  
  Aidha, kocha huyo amewateremsha hadi kikosi cha pili wachezaji wengine watano ili kuwapa nafasi nyingine ya kujibidiisha na kukuza uwezo wao.
  Tavares haridhishwi na uwezo na mwenendo wa John Kinabo, Kassim Simbaulanga, Abdulrahman Mussa, Mohd Babu na amewapeleka timu B wajirekebishe.
  Mohamed Fakhi aliyesajiliwa kutoka Simba SC amefukuzwa African Lyon kwa utovu wa nidhamu

  Na Mkurugenzi wa African Lyon, Rahim Kangenzi ‘Zamunda’ amesema hawezi kuingilia maamuzi ya benchi la ufundi.
  “Hatuwezi kuingilia uamuzi wa benchi la Ufundi, wao ndiyo wanajua kila kitu kwa wachezaji, hivyo sisi tunaafiki yote wanayoamua,”amesema leo Zamunda.
  African Lyon iliyoanza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa sare ya 1-1 na Azam FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam Jumapili itamenyana na mabingwa watetezi, Yanga SC. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KOCHA MRENO WA AFRICAN LYON AMFUKUZA BEKI WA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top