• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 30, 2016

  KIIZA DIEGO ATUA FREE STATE STARS YA AFRIKA KUSINI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba SC, Hamisi Kiiza 'Diego' yuko mbioni kujiunga na Free State Stars ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
  Nyota huyo wa Uganda yuko Afrika Kusini tangu mwishoni mwa wiki akifanya mazoezi na timu hiyo ya Bethlehem na anatarajiwa kusaini Mkataba wa mwaka mmoja kuanzia leo.
  Free State Stars imemtaka kwanza Kiiza kuhakikisha Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) inapatikana kutoka Tanzania alikocheza Simba SC msimu uliopita ndipo wasaini naye Mkataba.
  “Kiiza anakwenda mbio kuhakikisha ITC yake inapatikana ili aweze kusaini Mkataba Free State,”kilisema chanzo jana. 
  Kiiza alifanya vizuri katika msimu uliopita akiwa na Simba SC baada ya kufunga mabao 24 kwenye mashindano yote, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC).
  Lakini pamoja na kuwa mfungaji bora wa timu msimu uliopita, Kiiza hakuongezewa Mkataba na kuondoka Msimbazi na Simba kuendeleza desturi yake ya kuwatupa wachezaji nyota naada ya awali kumtema aliyekuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu, Mrundi, Amissi Tambwe. 
  Tambwe ameendeleza makali yake ya kufunga hata baada ya kuondoka Simba SC, kwani akiwa Yanga SC msimu huu ameibuka tena mfungaji bora wa Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIIZA DIEGO ATUA FREE STATE STARS YA AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top