• HABARI MPYA

  Jumapili, Agosti 28, 2016

  ULIMWENGU KURUDI UWANJANI NUSU FAINALI AFRIKA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu amesema kwamba anatarajia kuanza kucheza tena Kombe la Shirikisho Afrika katika hatua ya Nusu Fainali baada ya kukosa mechi zote za mzunguko wa pili za Kundi A.
  Ulimwengu hakucheza mechi za mzunguko wa pili Kundi A, dhidi ya Medeama nchini Ghana, MO Bejaia nchini Algeria na Yanga SC mjini Lubumbashi kutokana na kuwa majeruhi, lakini sasa yuko fiti.
  “Kwa kweli kwa sasa nipo fiti kabisa na tupo tunaendeleaa na maandalizi ya Nusu Fainali. Bila shaka nitacheza kuanzia Nusu Fainali,”alisema Ulimwengu akizungumza kutoka Lubumbashi.  
  Ulimwengu anatarajia kuanza kucheza tena Kombe la Shirikisho Afrika katika hatua ya Nusu Fainali 

  Baada ya kuongoza Kundi A, Mazembe itamenyana na Etoile du Sahel ya Tunisia wakati MO Bejaia itamenyana na FUS Rabat ya Morocco katika Nusu Fainali mechi za kwanza zikichezwa wikiendi ya Septemba 16 hadi 18, wakati marudiano yatakuwa wikiendi ya Septemba 23 na 25.
  Akizungumzia mechi na Etoile, Ulimwengu alisema; “Itakuwa mechi ngumu, Etoile ni moja kati ya timu bora sana katika mashindano haya, tunatarajia uponzani wa ndani nan je ya Uwanja, ila tutapambana,”alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ULIMWENGU KURUDI UWANJANI NUSU FAINALI AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top