• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 23, 2016

  BEJAIA WATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

  TIMU ya Mouloudia Olympique de Bejaia imefanikiwa kwenda Nusu Fainali Kombe la Shirikisho la Afrika baada ya kuifunga 1-0 Medeama ya Ghana Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia.
  Bao pekee la ushindi la wenyeji limefungwa na kiungo raia wa Chad, Morgan Betorangal dakika ya  akimalizia pasi ya Kamel Yesli.
  Bejaia inafanikiwa kumaliza nafasi ya pili kwenye Kundi A kwa pointi zake nane, sawa na MO Bejaia na inafuzu kwa sababu katika mechi mbili dhidi ya Medema ilivuna pointi nne, baada ya sare katika mchezo wa kwanza Ghana.
  Bejaia inaungana na vinara wa kundi hilo, Mazembe waliomaliza na pointi 13, wakati Yanga ya Tanzania imeshika mkia kwa pointi zake nne.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BEJAIA WATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top