BARCELONA imeilipua mabao 3-2 Villarreal katika mchezo wa La Liga usiku wa jana Uwanja wa Nou Camp.
Denis Cheryshev alianza kuwafungia wageni Villarreal dakika ya 30, kabla ya Neymar kuisawazishia Barcelona dakika ya 45.
Dario Vietto akaiaweka mbele tena Villarreal kwa bao la dakika ya 52 kabla ya Rafinha kuisawazishia Barcelona kwa mara ya pili dakika ya 53.
Shujaa wa mechi ya jana alikuwa ni Mwanasoka Bora wa zamani wa dunia, Messi aliyeifungia Barcelona bao la tatu dakika ya 56.
Kikosi cha Barcelona kilikuwa; Bravo, Pique, Mascherano, Alba, Alves; Busquets/Mathieu dk72, Iniesta, Rafinha/Rakitic dk88, Suarez/Pedro dk79, Messi na Neymar.
Villarreal; Asenjo, Gaspar, Musacchio, Ruiz, Costa, Pina/Trigueros dk77, J Dos Santos/Gomez dk85, Cheryshev, Soriano, Vietto na G Dos Santos/Uche dk89.
Rafinha (kaikati) akipongezwa na wote Neymar (kushoto) na Messi baada ya kuifungia Barcelona bao la pili la kusawazisha
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2935562/Barcelona-3-2-Villarreal-Lionel-Messi-scores-wonderful-winner.html#ixzz3QZ77jmEb
0 comments:
Post a Comment