// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MALINZI AWAPA POLE MISRI BAADA YA VURUGU ZILIZOSABABISHA MASHABIKI KUFIA UWANJANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MALINZI AWAPA POLE MISRI BAADA YA VURUGU ZILIZOSABABISHA MASHABIKI KUFIA UWANJANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, February 10, 2015

    MALINZI AWAPA POLE MISRI BAADA YA VURUGU ZILIZOSABABISHA MASHABIKI KUFIA UWANJANI

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Shirikisho Soka Tanzania  (TFF) amepeleka salamu za rambirambi kwa Rais Mohamed Gamal wa Chama cha Soka Misri (EFA ), kufuatia vifo vya mashabiki vilivyotokea mwishoni wa wiki katika mchezo uliowakutanisha  Zamalek na ENPPI.
    Mashabiki wapatao 22 wameripotiwa kupoteza maisha katika vurugu hizo zilizowahusisha mashabiki wa Zamalek na ENPPI na kusababisha Shirikisho la Soka Misri kuisimamisha michezo ya Ligi nchini humo.
    Katika salamu zake, kwa niaba ya TFF, familia ya mpira wa miguu na Watanzania, Rais Malinzi amewaomba wapenzi wa soka nchini Misri kuwa wavumilivu  katika kipindi hiki cha maombelezo ya vifo vya mashabiki hao.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi (katikati) amewapa pole Misri

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALINZI AWAPA POLE MISRI BAADA YA VURUGU ZILIZOSABABISHA MASHABIKI KUFIA UWANJANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top