Na Vincent Malouda, NAIROBI
MABINGWA wa ligi kuu ya taifa la Kenya, Gor Mahia, wameanza vyema kampeni ya michuano ya Kombe la klabu bingwa barani Afrika kwa kuwacharaza CNaPS Sports kutoka Madagascar 1 – 0 katika mechi ya raundi ya kwanza iliyogaragazwa uwanjani Nyayo, Nairobi.
Kiungo Victor Ali Abondo aliyewapa kombe la Super Cup katikati mwa juma kwa kufunga mabao mawili ndiye tu aliyefunga bao hilo la kipekee katika dimba la leo mnamo dakika ya pili baada mlindamlango wa CNaPS Randrianasolo kumchezea madhambi straika chipukizi Michael Olunga eneo la hatari.
Abondo alimtuma Randrianasolo upande wa kulia akiuwekeza mpira huo mfu upande wa kushoto pembezoni mwa lango na kuwaamsha halaiki ya mashabiki wa Gor Mahia alimaarufu K’Ogalo waliyobahatika kufika uwanjani.
Timothy Otieno alikuwa na nafasi nyengine ya kufanya mambo kuwa 2 - 0 dakika ya 22 lakini shuti lake liliugonga mwamba na kutoka nje.
Wageni walipata nafasi ya kwanza mchezoni dakika ya 37 kupitia Simouri lakini shuti lake halikumshtua golikipa wa Gor Mahia Boniface Oluoch, kipindi cha kwanza Gor wakiongoza 1 - 0.
Mambo yaliwaendea mrama mabingwa hao wa Madagascar kipindi cha pili huku wakipoteza nafasi za wazi licha ya kuwapendeza mashabiki kwa kutesa mchezo wa kitabu akili na ubongo. Dakika ya 81, Nono Vombola alishindwa kutumia makosa yaliyofanywa na mabeki wa Gor Mahia kwa faida yake kwani juhudi zake za kufunga ziliambulia patupu baada ya kipa Oluoch kutoka nje ya lango lake na kuokoa shambulizi hilo la moja kwa moja.
CNaPS walizidi kuonyesha mchezo mzuri licha ya kucheza ugenini lakini walishindwa kupata bao la kuzawazisha katika dakika nne za mazidadi, refa mzawa wa Uganda Dennis Batte akimaliza ngarambe hiyo.
Timu zote mbili zitamenyana tena katika mechi ya marudiano majumaa mawili yajao huku Gor ikihitaji sare yoyote kupenyeza awamu ya ijayo.
Kikosi cha Gor Mahia kilikuwa: 23. Boniface Oluoch (GK), 5. Musa Mohammed (Nahodha), 4. Kevin Oluoch, 26. Glay Dirkir, 2. Godfrey Walusimbi, 10. Khalid Aucho, 8. Jerry Santo (17. Eric Ochieng’ 55’), 7. Ronald Otieno Omino, 30. Ali Abondo, 9. Timothy Otieno (25. George Odhiambo 64’) 19. Michael Olunga
Kikosi cha CNaPS Sports: 16. Randrianasolo (GK), 22. Andoniaina Rakotondrazaka, 18. Toby Njakanirina (Nahodha) 4. Feno Ratolojahanary, 17. Rajaonarivelo, 12. Njiva Rakotohalihalala (11. Jean Andriamangason 68’), 20. Ramanitrandsana. 5. Michael Rabeson. 9. Nono Vombola, 7. Simouri (3. Olivier Ralaidimy 59’)
Kwingineko, KCC FC ya Uganda iliwalaza Cosmos de Bafia ya Cameroon 1 – 0. Bao la kipekee likifungwa na Herman Wasswa mnamo dakika ya 85 katika mtanange uliyoandaliwa uwanjani Namboole, mjini Kampala, Uganda.

0 comments:
Post a Comment