KLABU ya Aston Villa imemteua Tim Sherwood kuwa kocha wake mpya katika Mkataba wa hadi mwishoni mwa msimu wa 2018.
Kocha huyo Mkuu wa zamani wa Tottenham Hotspur atakuwa jukwaani wakati Villa inamenyana na Leicester Jumapili kabla ya kutambulishwa katika Mkutano na Waandishi wa Habari Jumatatu.
Sherwood anakabiliwa na jukumu la kurejesha makali ya timu hiyo ambayo imecheza mechi 10 za Ligi Kuu ya England bila kushinda, huku wakiwa kwenye hofu ya kushuka daraja.
Aston Villa imemthibitisha kocha wa zamani wa Tottenham Hotspur, Tim Sherwood kuwa kocha wao mpya
0 comments:
Post a Comment