// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); CHANONGO AFUNGIWA MECHI TANO NA FAINI JUU KWA KUPIGA REFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE CHANONGO AFUNGIWA MECHI TANO NA FAINI JUU KWA KUPIGA REFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, January 20, 2015

    CHANONGO AFUNGIWA MECHI TANO NA FAINI JUU KWA KUPIGA REFA

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    WINGA wa Simba SC, Haruna Chanongo anayecheza kwa mkopo Stand United ya Shinyanga, amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya Sh. 500,000.
    Chanongo amepewa adhabu hiyo kwa kuzingatia Kanuni ya 37(3) ya Ligi Kuu baada ya kumpiga teke mwamuzi wa mechi dhidi ya Polisi Morogoro iliyochezwa Januari 3 mwaka huu Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
    Kwa ujumla, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imewapiga faini na kuwafungia mechi wachezaji wawili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa kufanya vitendo kinyume na kanuni zinazotawala ligi hizo.
    Haroun Chanongo amefungiwa mechi tatu na faini juu 

    Kipa wa zamani wa Simba SC, Amani Simba anayechezea Oljoro JKT kwa sasa, amepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kukataa kupeana mkono na viongozi wakati wa kusalimia kabla ya kuanza mechi kati ya timu yake na Toto Africans iliyofanyika jijini Mwanza. 
    Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa kanuni ya 14 ya FDL. Timu ya Polisi Mara imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na vurugu za washabiki wake wakati wa mechi ya FDL dhidi ya Mwadui ya Shinyanga iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma. Pia Polisi Tabora imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na vurugu za washabiki wake kwenye mechi namba 40 dhidi ya Geita Gold, adhabu ambazo zimetolewa kwa mujibu wa kanuni ya 41.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHANONGO AFUNGIWA MECHI TANO NA FAINI JUU KWA KUPIGA REFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top